Thursday, December 23, 2010

UMECHAGULIWA JINSI ULIVYO,JIKUBALI

UMECHAGULIWA JINSI ULIVYO, JIKUBALI HIVYO

1 Wakorintho 1:18-31
“18Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19Kwa maana imeandikwa: “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima na kuzibatilisha akili za wenye akili.” 20Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa umpumbavu? 21Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua Yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale waaminio kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. 22Wayahudi wanataka miujiza na Wayunani wanatafuta hekima, 23lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulibiwa, ambaye kwa Wayahudi ni kitu cha kukwaza na kwa Wayunani ni upuzi. 24Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, yaani, Wayahudi na Wayunani, Kristo ni nguvu na hekima ya Mungu. 25Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu. 26Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi waliokuwa na nguvu, si wengi waliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. 27Lakini Mungu alichagua vitu vipumbavu vya ulimwenguni ili aviaibishe vyenye hekima, Mungu alichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili aviaibishe vyenye nguvu. 28Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, 29ili mtu ye yote asijisifu mbele za Mungu. 30Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi, 31ili kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”

1. Kuchaguliwa maana yake nini-
Mpendwa wangu, napenda nikwambie haya maneno yaliyo katika kichwa cha ujumbe huu kwa mara nyingine tena baada ya kuyasoma hapo juu, umechaguliwa jinsi ulivyo kazi yako kubwa ni kujikubali jinsi ulivyochaguliwa. Nimechaguliwa jinsi nilivyo na ninajikubali hivyo pia na napenda wote mnaosoma hapa mjue kuwa tumechaguliwa jinsi tulivyo na ni muhimu kujikubali jinsi tulivyo. Kabla sijafika mbali napenda kusema maana ya haya maneno ili tunapoendelea tuwe katika kiwango kimoja cha uelewa, shauku yangu ni kuona haya maneno yanakuvusha kwenda hatua na kiwango cha juu, kile kiwango alichokusudia Mungu mwenyewe,kiwango cha wewe kujijua na hata kufika mahali ukajivunia kuwa jinsi ulivyo. Kiwango cha kukupa nguvu ya ushindi ujapopita katika kudharauliwa, kukataliwa, kutengwa, kubezwa, kusimangwa na hata kuabishwa. Amin nakwambia ukijua siri hii, utavuka na kushinda mengi sana yanayoletwa kwako kukuletea dhihaka. Na neema ya Mungu ipo kukusaidia kuelewa katika jina la Yesu. Wengi wamepotea kwa kukosa ufahamu sahihi wa wao ni akina nani na wanatakiwa waishi maisha ya namna gani mpaka wakajikuta wananunuliwa kwa vitu dhaifu na vinyonge sana. Kwa hiyo nataka kwanza nikazie kusema umechaguliwa jinsi ulivyo, umechaguliwa na udhaifu wako na uwezzo wako. Kuchaguliwa ni kuchaguliwa tu.

Maneno ya msingi hapa ni umechaguliwa na jikubali na haya ndo yamejenga msingi wa yote yaliyo humu ndani ya maandishi haya. Najua kuwa wote tunaelewa maana ya neno umechaguliwa au chagua au kuchaguliwa, yote mzizi wake ni neno chagua. Chagua au kuchagua ni kufanya maamuzi ya jambo lolote kutegemeana na hali ya mtu mwenyewe, kwa mfano mimi nikikuchagua wewe kuwa rafiki yangu maana yake nimeamua kukufanya rafiki bila kujali mtizamo wa mtu yeyote wa nje. Hapo nakuwa nimeangalia hali yangu ya ndani na vitu kama upendo wangu kwako na mambo ambayo yananivutia mimi binafsi. Hivyo uchaguzi ni jambo la binafsi sana, kwahiyo mimi nikikuchagua hata kama utasikia maneno yasiyoendana na uchaguzi wangu kwako,hayo maneno hayabadilishi ukweli wa kwamba mimi nimekuchagua. Kwa lugha nyingine ukichaguliwa na mtu,hakuna mtu anayeweza kuja kubadilisha kuchaguliwa kwako. Watu pekee wanaoweza kubadilisha huo uchaguzi ni wewe na aliyekuchagua, kama aliyekuchagua amesema amekuchagua basi hiyo itaendelea hivyo milele ingawa uliyechaguliwa unaweza kukataa na kutokukubali kuwa umechaguliwa.

Ujinga ndo jambo kubwa sana linalopelekea mtu kuishi kama kichaa, bora hata kichaa maaana anajua anatakiwa apitepite mitaa ya majalalani ili apate chakula. Ni muhimu kujua huu msingi mpendwa wangu. Kutokujua mambo na kutotaka kujifunza kujua kumewafanya wengi wajiharibu matumizi yao. Ukichaguliwa umechaguliwa, lakini unaweza ukachaguliwa bila kujua ambayo haitazaa matunda sana. Kumbe msingi mwingine wa kuchaguliwa ni kujua umechaguliwa. Kuna utofauti kama nikikuchagua bila kukwambia na kama nikikuchagua na nikakwambia. Kujua kwamba nimekuchagua kuna nguvu zaidi ya kutokujua.Kuchagua jambo ni maamuzi ya mtu binafsi,na ndio maana wengi waliochaguliwa vitu mbali mbali wanayo mengi ya kusema kuhusiana na mambo waliyokutana nayo. Wengi huogopa kufanya maamuzi ya kuchagua kwa sababu hawataki kuwajibika kwa maamuzi yao bila kujua kuwa kuwajibika ndio raha ya kufanya maamuzi. Mfungwa aliyezoea kukaa jela, anaweza akagoma kuja kuishi uraiani kwa sababu ameshazoea kula kilaini na hataki tena kuwajibika na kufanya kazi halali, utumwa ni mbaya ndugu. Kwa hiyo hiyo ndo mtizamo wangu wa neno umechaguliwa lakini nataka twende hatua ya ndani zaidi hapa.

Siku moja nikiwa kanisani niliwahi kumuuliza mwana wa Mungu mmoja juu ya habari ya Marafiki na nikamuuliza nani ni rafiki yake wa dhati au best friend, akanitajia jina la msichana ambaye wamekuwa nae wote mara nyingi na mpaka watu wanaona kuwa wao ni Marafiki wa kweli. Nikamuuliza kama rafiki yake huyo anajua kama yeye ndiye best friend kwake akasema hana uhakika lakini hivyo ndivyo ilivyo. Nikaendelea na uchunguzi, wakati mwingine nikamwita Yule rafiki aliyetajwa kuwa ndo best naye nikamuuliza rafiki yake wa karibu. Huyu cha ajabu akanitajia jina la rafiki mwininge kabisa na wala sio Yule aliyemtaja. Siku nyngine nikamuuliza Yule wa kwanza utajisikiaje kuwa rafiki unaesema ndio best hajuia kama wewe ndiye best na yeye ana rafiki yake best mwingine? Akasema atajisikia vibaya sana. Inauma sana, kuchagua au kuchaguliwa bila kujua. Pamoja na kwamba unaweza ukawa umechaguliwa bila kujua hiyo haibadilishi ukweli kwamba umechaguliwa maana kama ni maamuzi yameshafanyika.

2. Fahamu kuwa umechaguliwa-Yohana 15:16

“Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi;”
Je, unafahamu au unajua kuwa wewe umechaguliwa? Swali litakalofuata hapo ni je, umechaguliwa na nani? Narudia tena kuwa mpendwa wangu umechaguliwa jinsi ulivyo, jikubali jinsi ulivyo na hakuna namna unaweza kupingana na huu ukweli zaidi sana wote wanaopingana na ukweli huu hali zao hazina matumini sana. Kwa vijana hali ni mbaya zaidi kwa maana kutojua wao ni akina nani kumewafanya waishi maisha ya kuigiza, maisha ya kuangalia video na sinema na kisha kufanya kama walivyoona au walivyosikia. Ukiona mtu yeyote anaishi maisha yasiyo halisi, tambua kuwa yuko kwenye hali ngumu sana ya kutokufahamu haya mambo. Kuishi maisha ya kuigiza ni ishara ya wazi kabisa ya kutojijua wewe ni nani, ni ishara ya kuonyesha kuwa huna thamani na wala huna jambo lolote jema linaloweza kuwafaa wengine kwa hiyo unaamua kuishi maisha ya kuigiza (Copy and Paste Lifestyle). Misha haya ya CPL ni maisha magumu sana maana ni maisha ya utumwa wa maamuzi ambayo yataendelea kuwepo mpaka mtu atakaporudi kwenye msingi wa chanzo chake na kutaka kujua zaidi juu ya yeye ni nani.

Kuna utofauti mkubwa sana kati ya kujua na au kutokujua kuwa umechaguliwa, ni sawa na kusema kuna faida ambazo zinaambatana na kujua na pia kuna hasara za kutokujua, hii ni kwenye jambo lolote katika maisha yako. Ukiwa umezaliwa na humjui baba yako ni tofauti sana na kama siku ile unapojua kuwa Fulani ni baba yako. Watu wengi na hasa vijana wanaishi katika kutokujua mambo mengi sana yanyowazunguka na ndio maana wengi ni mawindo ya ibilisi kwa kutumia vyombo vya habari na Marafiki. Nataka ufahamu kuwa Mungu ndiye amekuchagua kupitia mwanawe Yesu Kristo, kwa hiyo fahamu umechaguliwa. Wengine wanafahamu wamechaguliwa na watu mbali mbali, wengine na dunia na starehe zake, wengine wamechaguliwa na nguvu za giza na mapepo na ni waaminifu sana kutumikia uchaguzi huo. Ninachotaka ufahamu hapa ni kwamba umechaguliwa ingawa kufahamu tu kuwa umechaguliwa haitoshi, ni muhimu kwenda hatua nyiningine ya kumfahamu aliye kuchagua. Je, unamjua aliyekuchagua?


3. Mfahamu aliyekuchagua
Unakumbuka ule mfano wa mwanzo? Ngoja niurudia hapa ili unielewe zaidi. Siku moja nikiwa kanisani niliwahi kumuuliza mwana wa Mungu mmoja juu ya habari ya Marafiki na nikamuuliza nani ni rafiki yake wa dhati au best friend, akanitajia jina la msichana ambaye wamekuwa nae wote mara nyingi na mpaka watu wanaona kuwa wao ni Marafiki wa kweli. Nikamuuliza kama rafiki yake huyo anajua kama yeye ndiye best friend kwake akasema hana uhakika lakini hivyo ndivyo ilivyo. Nikaendelea na uchunguzi, wakati mwingine nikamwita Yule rafiki aliyetajwa kuwa ndo best naye nikamuuliza rafiki yake wa karibu. Huyu cha ajabu akanitajia jina la rafiki mwininge kabisa na wala sio Yule aliyemtaja. Siku nyngine nikamuuliza Yule wa kwanza utajisikiaje kuwa rafiki unaesema ndio best hajuia kama wewe ndiye best na yeye ana rafiki yake best mwingine? Akasema atajisikia vibaya sana. Inauma sana, kuchagua au kuchaguliwa bila kujua.

Hili swali ni muhimu sana, umechaguliwa na nani na kwanini? Ni muhimu kujua umechaguliwa na nani maana maisha yetu hapa duniani ni maisha ya kuchagua. Sisi wenyewe tunavitu vingi tulivyochagua wenyewe na sasa hivi hivyo vitu ni mali yetu. Mke anamchagua mume na mume anamchagua mke, anaechagua ana nguvu zaidi ya yule anaechaguliwa. Nini nasema hapa? ukisoma Neno la Mungu utaona linasema waziwazi kuwa sisi tumechaguliwa toka mwanzo na pia kuwa sisi tunampenda Mungu kwasababu yeye ndo aliyeanza kutupenda kwanza. Hamna mtu aliyejichagua mwenyewe kama vile hakuna aliyejiumba mwenyewe. Asili yetu ni Mungu mwenyewe kwa maana alituumba kwa sura yake na mfano wake.

Ukienda dukani kunua nguo au simu ni kitu gani kinakufanya uichague nguo au simu Fulani na kuiacha nyingine wakati ziko nyingi tena za aina mbali mbali? Kitu gani kinakufanya umchague rafiki huyu na kumuacha huyu? Je unajua kuwa uchaguzi unahusisha pande mbili, yaani upande unaochagua na ule unaochaguliwa? Kwa mfano ukienda sokoni kununu nyanya utakuta mafungu kadhaa yamepangwa mezani na kati ya hayo wewe mchaguaji unataka fungu moja. Kwahiyo kwa upande mmoja wewe unachagua fungu la nyanya utalooona linakufaa na kwa upande mwingine hilo fungu la nyanya litawakilishwa na muuzaji kukubaliana nawe kwa misingi ya bei iliyopangwa. Kwahiyo uchaguzi ni maamuzi na kila uchaguzi una gharama zake. Kuna gharama za kuwa na rafiki uliyenae sasa, kama hukulipa mwanzoni mwa urafiki basi unalipa sasa au utalipa baadae, cha msingi ni kuwa ni lazima ulipe gharama ya kufanya maamuzi ya kuchagua.

Yohana 15:16 inasema “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi… “Aliyetufia ndiye aliyetuchagua. Tumechaguliwa na Mungu, aliyeziumba mbingu na nchi, umechaguliwa na Bwana wa majeshi, Mfalme wa utukufu, Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana wote unaowajua na hata wale usiowajua. Tumechaguliwa ndani yake Kristo Yesu, ili tuwe na urithi katika ulimwengu huu na ujao pia, ametuchagua tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. Efeso 1:11.

4. Unajisikiaje kujua umechaguliwa na Mungu

Zaburi 34:8 inasema, “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema, heri mtu Yule anayemtumaini”
Hebu nikuulize swali, ulishawahi kujidharau, kumdharau mtu, kudharauliwa? Ulishawahi kujiona hauna maana na haufai hata kufika mahali ukataka kujiua au kwenda kujificha porini?. Ulishawahi kujilinganisha na rafiki yako,au ulishawahi kutamani kuwa kama rafiki yako,kuvaa mavazi kama yake, simu yake,wazazi wake,mali zake na hata muonekano au haiba yake? Ulishawahi kukataa kufanya jambo Fulani uliloambiwa ulifanye kwa kutojiona wewe huwezi kulifanya? Hapa kuna maswali mengi sana ya kujiuliza na yote yatajibiwa katika waraka huu. Mimi binafsi nimeshapita kwenye vipindi mbalimbali vya maisha kama maswali haya yalivyouliza. Kuna wakati nilijiona nimezaliwa kwenye ukoo duni, familia duni, mkoa duni na hata nikakua kwenye mazingira magumu sana. Pia nimeona watu wengi wengi sana wakishindwa kufanya na hata kutofikia malengo yao katika maisha kwasababu ya kupita katika vipindi mbali mbali sawasawa na maswali hayo hapo juu.

Kadri utakavyokuwa unasoma utaona majibu ya maswali mengi ulonayo moyoni na mpaka ujue ni kwanini watu wengi wanafika mahali wanajiona hawafai na hawana msaada wowote katika jamii. Fahamu kuwa kupita kwenye maisha magumu na yanayokatisha tamaa na kuishia hapo haitoshi, ni lazima uvuke upande wa pili ambao ndio msingi wa yote nitakayoyasema hapa. Watu wengi wamepita katika maisha hayo, wengi wamebaki katika hali hizo na wachache wameenda mpaka upande wa pili. Wengi wamekatishwa tamaa na ndugu na jamaa wa karibu na wamekubali hiyo hali mpaka sasa wanateswa na hiyo hali. Wengi wametukanwa na kutamkiwa maneno magumu juu ya maisha yao kiasi kwamba wanaona hakuna umuhimu wa kuishi. Wengi wamehubiriwa injili ya mapepo, wengi wanajiona wana laana, wana mikosi, wana nuksi kumbe nuski ni ufahamu wao wenyewe.

Ngoja niseme hap akuwa umechaguliwa na Mungu, Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, mwenye nguvu zote. Haujachaguliwa na waziri mkuu, rais, mwalimu mkuu wa shule, kiranja, baba wala mama bali umechaguliwa na Mungu mwenyewe. Unajisikiaje kuchaguliwa na Mungu mwenyewe? Unajisikiaje kujua kuwa Mungu ndiye aliyekuchagua na kwamba hakuna anayeweza kubatilisha uchaguzi wake? Kisiasa watu hukataa matokeo ya uchaguzi na kwenda mahakamani, lakini hao ni wanadamu, nani atakaempinga Mungu kwamba amekuchagua? Yeye ndiye mwenye haki na ufalme wa ke unatangaza Furaha, amani na haki katika Roho Mtakatifu. Warumi 14:17.

5. Aina gani ya vitu au watu vi(wa)mechaguliwa na Mungu
Ukisoma 1 Wakorintho 1:26-29 utapata jibu la moja kwa moja kuhusu aina ya vitu alivyovichagua Mungu. Nitakusaidia kuvitaja hapa na kukuelezea kidogo ili usije uakatafuta sababu ya kubaki na kuishi maisha katika ujinga. Lakini ili unielewe vizuri ngoja nianze kusema vitu au watu ambao Mungu hajavichagua au hajawachagua.
• Si wengi wenye hekima ya mwilini
• Si wengi wenye nguvu
• Si wengi wenye cheo
• Si wengi wenye fedha na utajiri
• Si wengi wenye historia nzuri za maisha yao
• Si wengi wenye sura nzuri na za kuvutia
• Si wengi wenye elimu,

Na listi inaendelea na hawa wote si wengi wao walioitwa ingawa huenda kabisa kuna wachache wao walioitwa. Hapo hebu tujiulize swali, wengi walioitwa ni watu wa namna gani sasa kama hao wote sio wengi walioitwa? Hili swali nalo linajibika vizuri kabisa, biblia inasema Mungu amechagua vitu vifuatavyo:
• Mambo mapumbavu
• Vitu dhaifu
• Vitu vinyonge
• Vitu vilivyodharauliwa
• Vitu ambavyo haviko
• Watu wasiofahamika
• Watu wasiovutia
• Watu wasio na elimu
• Wasiotoka kwenye familia bora

Na hata hapa mlolongo ni mrefu kuutaja, lakini hata kwa mifano unaweza kujifunza, kwa mfano: Musa alitoka wapi, mfalme Daudi je, Nabii Isaya, Yeremia au Daniel? Vipi kuhusu Yesu mwenyewe? Mtoto wa fundi seremala, anachezea mbao, nani alimjua? Vipi kuhusu wewe mwenyewe unaesoma hapa? Kumbuka nyuma kidogo, tangu umezaliwa, ukakua na ukaenda shule ya msingi, secondary mpaka hapo ulipofika ni watu wangapi umewaacha njiani na wengine hata hujui wako wapi, wewe ni nani? Kwanini uchagulliwe na Mungu na una thamani gani? Nilipojua hii siri kwamba Mungu amenichagua na udhaifu wangu, na yote niliyonayo nilianza ukurasa mpya katika maisha yangu.

6. Ufahamu wa Ki-Mungu unakupa kujua thamani yako

Warumi 1:28 inasema, “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.”
Ukiendelea kusoma misitari iliyobakia utashangaa sana. Faida za kukataa kuwa na Mungu katika fahamu za mtu zimetajwa waziwazi nazo ni:
• Kujawa na udhalimu wa kila namna
• Uovu na tama mbaya
• Kujawa na husuda, uuaji, fitina, hadaa
• Kuwa na nia mbaya
• Kusengenya
• Kusingizia
• Kumchukia Mungu
• Kuwa na jeuri
• Kutakabari
• Wenye majivuno
• Kutunga mabaya
• Wasiowatii wazazi wao
• Wasio na Rehema
• Wachochezi

Anything has a price to either pay or receive. When you receive it simply means that you are being bought by and if you are paying it means that you are buying something. Price is how much needed to get something or loose something. Price is both way, receiving and giving. But value determines price-that is how much a book is sold depends completely on the value it carries. Value is determined by various things that have been used to make up something; these are materials used or ingredients or contents. This simply means how scarce or plentiful those materials are, that is how much value the product will have. In most cases, where there is no value there is no price. Value is both internal and external and there is a big difference between having certain values and knowing that you have them. Most of the things that people don’t know their values are priceless or cheap, this applies to everything including people. Knowing how worthy you are will make you in the position to even determine your price.

For example, in labor market where price is given according to merit and other qualifications, you easily know how much to pay someone with a certificate, a diploma, a degree or masters. Here education becomes one of the ingredients that make that job seeker and later his various abilities will be seen and used to promote and motivate. Beyond values and ingredients there is a source or the origin. The source determines everything, the source determine

Basically in our day to day dealings we pay our prices in regards to our choices we make. Economically, this idea is called opportunity cost. So we are sold and sell just as we buy and being bought. If I wake up in the morning and decided not to go to work-then my price is the very reason that made me not to go. If I did not go because of being lazy, then laziness is my price, got it? My value is connected to the vision and mission of God to me. Mission and vision of God is only found only in his heart and in his mind, moreover the heart and mind of God is demonstrated to what he speaks, I mean his word.

Lakini pia wengi wako tayari kununuliwa hata kwa chipsi (viazi vya kukaanga vilivyokatwakatwa), wengi wananunuliwa kwa pesa, mali, magari na vitu vinavyoonekana ni vya thamani sana. Wengi wamewauza ndugu zao kwa mizimu kwa sababu ya utajiri. Huu ni ukosefu wa akili, maarifa na hekima kwa kiwango cha juu sana. Tafsiri ya mambo yote haya ni kuwa, watu wengi hawajui thamani ya maisha yao na thamani yao wenyewe. Hebu jiulize wewe ni wa thamani gani. Ninachotaka kusema ni kuwa, kwa ujumla kuna hali ya kutojiamini, kujidharau, kudharauliwa ambayo ipo katika jamii na hasa ndani ya mwili wa Kristo. Kwa hiyo ni muhimu tukakumbushana tena kuwa, kila mtu amechaguliwa jinsi alivyo na inampasa kujibali hivyo alivyo. Swali la msingi hapa ni hili: Hayo yote yanatoka wapi?

7. Kwanini Mungu amekuchagua wewe
Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi nilyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.”

Nataka ujue hapa kuwa baada ya kujua hayo yote kwamba Mungu amekuchagua, ni muhimu sana kujua sababu au dhumuni au malengo au matarajio ambayo Mungu anayo ya kukuchagua wewe na majibu yake pia yako wazi kabisa kwenye kitabu hiki hiki cha wakorintho. Amekuchagua jinsi ulivyo ili:
• Ili kumzalia Mungu matunda yadumuyo
• Ili utumike kuwaaibisha wanajiona wana hekima
• Ili utumike kuwaaibisha wajionao kuwa wana nguvu
• Ili Mungu avibatilishe vitu vilivyoko kupitia wewe
• Umechaguliwa kwa sababu wewe ni mali yake
• Una chapa yake-sura na mfano wake
• Kwasababu ameamua kukuchagua

No comments: