Friday, June 18, 2010

HE NEEDED THE TWELVE-ALIWAHITAJI KUMI NA WAWILI

“Underscoring the significance of people as assets and resources in the fulfillment of one’s vision and purpose”
Baada ya kimya cha muda mrefu wa fungate na mambo kama hayo, napenda kuanza upya kabisa kuwaletea lile somo nililolikatisha kipindi Fulani huko nyuma linalosema ALIWAHITAJI 12 au HE NEEDED THE TWELVE. Mfululizo unaokazia sana umuhimu wa kuwa na watu sahihi katika kufika kilele cha utimilifu wa maono aliyonayo mtu yeyote kwa kutumia mfano wa Bwana wetu.Hivyo naongelea umuhimu wa kuwa na watu sahihi, thamani yao na kwa nini ni muhimu kujua ni namna gani ya kuishi na watu vizuri.Na hivyo napenda niseme machahe katika hicho kitabu kwa faida yetu. Kumbuka kuwa kila mmoja wetu hapa anamaono na mahali anakotaka kwenda na ili afike ni lazima apate watu watakaomsadia kufika huko. Na kwa namna moja au nyingine hakuna mtu anaeweza kutimiza maono au mipango yake yeye mwenyewe, hakuna. Tunategemeana sana na unaweza ukajiuliza pia kwa mfano, Marafiki huru imetoka wapi? Nani mwanzilishi? Unadhani mwanzilishi peke yake angeweza kuifikisha ilipofika? Unadhani watu wakiacha kujibu barua pepe zinazotumwa kila siku na Marafiki sehemu mbalimbali kutakuwa na uhai wa Marafiki huru? Au jiulize wewe mwenye binafsi ni watu wangapi wameshiriki kukufanya uwe jinsi ulivyo sasa na ufike ulipofika sasa?

Utaona na kushangaa sana kwamba kuna watu hata umeshawasahu lakini walichangia wewe kuwa hivyo ulivyo. Kuna watu unawakumbuka na usiku kucha unawaombea kwa jinsi walivyoshiriki kuyafanya maisha yako yawe hivi yalivyo. Kwa hiyo ni vema tukajifunza kwa undani juu ya jambo hili kwa maana ni muhimu kujua. Najua unajua kuwa hata Mungu mwenyewe anatafuta mtu ili aweze kuleta mabadiliko kwa eneo husika na ndio maana wewe upo hapo ili kuendelea kuyafanya yale ambayo aliyekuweka anataka ufanye. Ukiangalia kwenye jamii ya sasa utaona kuwa watu wanaosaidia jamii wanakibali sana duniani, watu waliogusa maisha ya watu kwa njia moja au nyingine hapa Tanzania na hata nje wanakibali sana mioyoni mwa watu. Hapa sizungumzii vyanzo vya misaada wanayotoa, nataka uone kuwa kufanya jambo kwa jamii kuna nguvu sana na ndio maana huwezi kujenga hospitali porini au uanzishe kanisa kwenye mbuga, ni vigumu sana. Umeshawahi kujiuliza wanasiasa wanachohangaikia ni nini? Kampeni zinafanyika ili iweje? Kwanini tupige kura ili mtu awe kiongozi? Kwanini rais anahitaji baraza la mawaziri, kwanini madiwani, wabunge na kwanini kuna wakati watu wakafikia mahali kusema wengi wape au the majority rules au kura ya veto?

Kuna mambo mengi ya kujifunza kuhusu watu na umuhimu wao. Fahamu kuwa hata kama unataka kunua shamba utawahitaji watu au mtu atakaekusaidia kupata shamba. Angalia kwa mfano unataka shamba maeneo ya Ruvu: unadhani asingekuwepo mtu kama Addo kutoa tu taarifa ya bei wa hekari moja huko ingekuwaje? Lakini ili tupate hayo mashamba kuna watu wengi sana wanatakiwa wahusishwe, watu kama mwenye shamba, serikali ya mtaa, mashahidi na hata walinzi. Labda tuangalie kwa kina zaidi hapa kwa mfano wa nyumbani. Hata kama mtu anahela kwa namna gani hawezi kuoa bila kuhusisha mtu hata mmoja, kwa sababu thamani ya helo hailingani ya thamani ya mtu, si unajua hata hela yenyewe kama haina mtu haina thamani? Unajua thamani ya wafanyakazi wa ndani? Watu walio na wajakazi wanajua, hata kama wewe ni bilionea lakini mfanyakazi wa ndani japo unamlipa elfu 25 lakini yeye anakusaidia kutimiza maono yako kwa kuilinda nyumba yako na watoto wako. Vipi kama umeenda kazini na kurudi unakuta nyumba imeteketea na document zako zote muhimu hazipo na watoto wako wote hawapo? Najua umeshawahi kusikia matukia kama hayo. Hiyo ndo thamni ya mtu na hakuna mtu asiye na thamni duniani.

Kila mtu ana thamani katika majira yake. Na ndio maana huwezi kuiona thamani ya Yuda Msaliti ukiwa hutaki wokovu au ukiwa unataka Yesu asiende msalabani. Kwa majira yake Yuda ambaye alichaguliwa na Bwana mwenyewe alikuwa ni wa thamani sana ili kusaidia kutimizwa kwa kusudi la ukombozi. Kwa hiyo kati ya wale 12 kila mmoja alikuwa na thamani yake iwe unajua au hujui. Wengine wanamsemaga vibaya Thomaso na imani yake ya kuona kwanza-seeing is believing badala ya imani ya kweli ya believing is seeing Hebrew 11. Lakini unajua zote mbili ni imani na tatizo sio imani yenyewe bali anaeitumia. Kwa wakati wake Thomaso alitufundisha kuwa kuna watu hawataenda mbele mpaka wameona, wana imani dhaifu na kuna wengine ni bulldozer na sio koleo. Kila mtu ana thamani kwa majira yake. Kwa majira yake namaanisha, huenda miaka mitatu nyuma mimi nisinge muhitaji Sasali au Addo au yeyote hapa lakini kwa majira na nyakati hizi nawahitaji wengi na ndio maana huwezi kuuona umuhimu na uthamani wa Yuda ukimuangalia baada ya ufufuo au wakati Bwana anazaliwa. Hata wewe kuna watu hawakuwaga na umuhimu walionao leo huko nyuma lakini kwa sasa ni kama dhahabu kwako. Kuna watu hivi leo tukisema tuwaondoe kwenye maisha yako hutakubali na hata ukikubali haitakuwa rahisi kama tungewachukua miaka mitano nyuma. Ni rahisi kumuacha mchumba kabla ya ndoa lakini baada ya ndoa unaelewa jinsi ilivyo ngumu. Unaweza kumchukia mtu mara ya kwanza ukimona lakini baada ya siku chache unaweza hata ukajitukana kwa kuwa hukujua uthamani uliojificha wa huyo mtu.ITAENDELEA....

By Raphael-Mindset Upgrade

No comments: