Friday, July 16, 2010

TAKE AWAY YOUR LIMITATIONS BY FORGIVING OTHERS

                                                     

Wapenzi wangu MH popote mlipo,ninawasalimu woote asubuhi hii kwa kupitia jina lenye nguvu la Bwana na Mwokozi wetu KRISTO YESU Mnazareth. Leo ni ijumaa nyingine ambayo nawaletea mwendelezo wa Mindset Upgrade yenye kichwa KWANINI NIKUSAMEHE.

Kabla sijasema mengi nitoe fursa kwa mtu yeyote ambae angependa kupokea Mindset Upgrade kwa njia ya mobile phone anitumie namba yake at 0787 110003.Mindset Upgrade ilianzia kwenye simu kabla sijaanza kuirusha huku kwenye email na ilianza karibia miaka minne iliyopita na sasa inapatikana kwa njia hii ya forum yetu ya marafiki huru.

KWANINI NIKUSAMEHE,naamini umeshajifunza mengi sana juu ya kusamehe na kusamehewa na leo nataka nikuongezee au nikupe namna nyingine ya kuona juu ya hili jambo.Kusamehe ni kutomuhesabia mtu hukumu kwa jambo ambalo amefanya kwa kukusudia au kutokukusudia.Ni kusahau na kuachilia.Na ninapenda sana kuelezea hili ili tujue nafasi ya kusamehe katika mafanikio yetu ya kila siku na mpaka ule uzima udumuo milele.Watu wengi wamekuwa si wepesi wa kusamehe pale wanapokosewa na watu na wengine ni wepesi sana wa kuwasamehe watu wanapowakosea.Utofauti uliopo kati ya hao watu ni utofauti kati ya kujua na kutokojua nguvu ya NEEMA ya Mungu maishani mwetu.Na leo nataka nielezee sababu tatu tu za kwanini tunatakiwa kusaheana.

Sababu zisizosahihi za kumsamehe mtu:Napenda nianze kwa sababu ambazo sio sahihi kuzitumia kumsamehe mtu:Usimsamehe mtu kwa sababu ni adui au rafiki yako,ni jirani yako, ni amekukosea sana, amekukosea kidogo,amekukosea mara chache au mara mia,ni mrefu au mfupi,ni mwembamba,kabila lake,umri wake.Ua kwa ujumla niseme hatutakiwi kuwasamehe watu kwa sababu ya mwonekano wao au makabila yao au namna tunavyoishi nao.Kuna dada mmoja kanisani wakati nafundisha juu ya somo hili akanambia,wewe kaka Rapha hujui tu yaani mtu anakukosea makusudi kabisa na hataki kuomba msamaha.

Tunatakiwa kusamehe iwe ni mtu ameomba au hajaomba msamaha,hii ndio KWELI na UKWELI ulio ndani yake.Watu wengi wamekuwa wakitembea na watu mioyoni mwao saana kutokana na kutokujua au kupuuzia uzito wa jambo hili la kusamehe.Mtu mmoja akanambia mimi sikusamehi mpaka baada ya masaa mawili,haha haha it is funny.Watoto hawataki kuwasamehe wazazi wao na wazazi hawataki kuwasamehe watoto wao. Kutokusamhe kumekuwa kwenye hali mbaya zaidi katika makanisa na hasa yanayoitwa ya kiroho.Mzizi huu wa kutokusamehe umeleta matokeo mengi mbalimbali na ndio maana mpaka leo kuna vitu haviishi makanisanio kama majungu, fitina,chuki,hasira,mifarakano,ufisadi na mambo meengi hata hayatoshi kuyaandika.

Nilishawahi kutuma Mindset Upgrade inayoongelea namna ambavyo watu wengi wamegeuza matumizi ya mioyo yao kuwa kama dustbins.Nikatoa mfano kusema, kitu kama UNFORGIVENESS doesnt belong to our hearts,na hivyo tukiweka kitu kisichotakiwa mioyoni mwetu tunabadili matumizi sahihi ya moyo.Kutokusamehe ni uchafu kama ukikaa moyoni, na hivyo nafasi yake ni kwenye dustbin na hivyo mtu aliyeujaza moyo wake na kutokusamhe moyo wake hauwezi kufanya kazi kwa usahihi na ufanisi kwa sababu software yake imekuwa corrupt.Moyoni kunapaswa kukaa vitu vinaitwa CHEMICHEMI ZA UZIMA na sio hila,majungu,chuki,kutokusamehe,wivu,majivuno,na mambo kama hayo.Kuyaweka hayo mambo moyoni ni kuubadili moyo kuwa eneo la kutupia takataka.Ngoja niishia hapa kwanza,niendelee na hizo sababu.

SABABU KUU TATU ZA KUMSAMEHE MTU:

1.Samehe kwasababu na wewe umesamehewa.Hakuna mtu hata mmoja kati yetu anayeweza kusema hajasamehewa dhambi zake na Mungu kupitia Mwanawe wa pekee yaani Yesu mwkozi.Wote tumesamehewa, yaani hata wayebusi na waperezi wamesamehewa pia,utofauti ni kujua na kutokujua na kuchukua hatua ufahamu huo.Kuna watu wanaishi kama hawajasamehewa.Dalili ya mtu aliyesamehewa ni ule moyo wake wa rehema na kupondeka anaokuwa nao baada ya kujua kuwa amesamehewa.Zaidi sana,Mungu ametusamehe kabla hata hatujaomba kusamehewa,ni sawa na kusema HE FORGAVE US IN ADVANCE,BEFORE WE ASK FOR IT HE GAVE IT TO US.
Ukisoma Mathayo 6:12 utaona imeandikwa,UTUSAMEHE DENI ZETU KAMA SISI NASI TUWASAMEHEVYO WADENI WETU,hii haimaanishi ukikopa utegemee kusamehewa,neno hapo ni deni ingawa tafsiri nyingine zinatumia neno makosa au maovu yetu.Ukijua kuwa hata wewe umesamehewa huwezi shindwa kumsamehe mwingine.Ukisoma maandiko ya Paul mengi utakutana na hili ninalolisema,nasi pia tulikuwa gizani wakati fulani huko nyuma kabla Nuru yake haijaangaza mioyoni mwetu na hivyo yatupasa kuwatendea wengine vile tulivyotendewa na Mungu kupitia neema yake.Hatukustahili kupendwa yeye akatupenda.Hatukustahili kusamehewa yeye akatusamehe kwa gharama zake wmenyewe.


No comments: