Tuesday, September 21, 2010

Papaa On Tuesday......Unaziba Tundu La Panya Kwa Kipande Cha Mkate?

Marafiki Huru Ni,
Ni matumaini Yangu Tuko wazima kwa kudra za Bwana Wetu Yesu Kristo. Nina kila sababu ya Kumshukuru Mungu Kutupa uzima katika kipindi hiki cha Kampeni za Uchaguzi lakini Pia tukiwa tumebakiza siku 4 tuingia pale Mlimani City Kwenye “Sifa Zivume”.


Juzi na Jana kwenye account yangu Face Book alijaribu kupata mawazo kutoka kwa watu kutokana na “Case” iliyokuwa mezani kwangu tangu alhamisi Jioni. Wanawake wengi sana hawapendi kudanganywa inapofika suala la mahusiano, iwe kabla ya ndoa ama baada ya ndoa, na wakati huo huo wanaume wengi sana wanashindwa kukizingatia kile kipengele cha kiapo kinachosema “Wengine Wote Nitawaepuka na kuambatana na wewe Siku Zote” hahahaha hapo bwana, unataka kujua?fanya tathimini Wake za Watu wangapi wako active kwenye Face Book na Wanaume za Watu wangapi wako active Face book na mitandao Jamii mingine. Kituko kingine ni vile Mpendwa mmoja amemshauri mchumba wake kwa hekima ajitoe kwenye Face Book, Tagged, Hi 5 na Twitter hii yote ni Mitandao Jamii pengine atamwambia ajitoe na Marafiki Huru kwa kuwa anahisi anaweza kuibiwa na Wajanja, Mdada kwa kujali na kutunza Mahusiano akaamua kujitoa ingawa ilikuwa ina muuma lakini “Fo The Sake Of Love” akawa hapatikani huko kote. Siku Ya Alhamis sijui niseme ni Mungu ama ni Machale baada ya kutuma picha za Marafiki Huru kwenye Net na zingine kuzipost katika Face Book na kwenye Blogs akaona ni vema akaangalie hizo picha akiwa Café. Alipofika Café akashawishika kuingia Face Book, akajiweka offline ili kutunza ndoa, kuangalia kati ya watu walio online Mchumba wake yuko online, akaamua kwenda kuangalia kwenye profile and photo comments za mtu wake, mmh akakuta yule kaka yuko full huru na Wana facebook, alipojaribu kwenda kwenye accont zingine za mitandao mingine since alikuwa na password akakuta password zimebadilirishwa teh akaona kama noma na iwe noma akajiweka online akaanza kuchat na mtu wake, swali la kwanza la Jamaa, kwanini umeingia Face Book?wakarumbanaaaa. Kesi bado inaendelea kwa sasa.

Ninachotaka kusema hapa sio tu ni namna gani watu wamekuwa sio waaminifu na wala sitafuti nani ni waaaminifu kuliko wengine kwenye mahusiano. Ila ninachotaka kukisema ni namna gani kwenye maisha tunataka kufunika mambo yaonekane ndivyo kumbe sivyo na tukusahau kunasiku yatakuja kutugharimu siku yakibainika. Nitatoa mifano michache ambayo inaweza kukugharimu kama utashindwa kujiweka huru Mapema. Marafiki Huru huwa tunaambiana ukweli, pale ambapo panapaswa kusemwa. Maisha yetu ya kila siku yanawaeza yakawa ni yakulipa gharama kila iitwapo leo kwa uongo ama ukweli tuliouficha wakati Fulani tukisahau kuwa utakuja bainika, maneno yetu ya kujificha ni kama kipande cha mkate kwenye shimo la panya ambapo kuna wakati mkate utaliwa tu.

Umesikia hizi issue sijui Tumaini Sio Raia sababu ana upara, Papaa Siojui kwao ni Congo ndo maana mfupi, kuna wakati mambo yetu yatawekwa bayana. Assume wewe unafanya kazi kwa kutumia Jina sio lako ama vyeti sio vyako, na umekuwa huru sana hapo ofisini, umewahi waza siku wakasema mwenye jina kama lako ameapply kazi teh teh. Unapotumia taarifa ambazo sio sahihi katika ajira kuna saa ya kulipa taarifa hizo. Jaribu kuwaza siku rafiki huru unatolewa kwenye TV kwenye taarifa ya habari kuwa huyu Jamaa alifahamika sana kama Papaa Sebene kumbe jina lake la kweli ni Asangalwisye Kandukungonde, ukitaka kugombea ubunge watu uliosoma nao wanasema tunamjua. Unapofunika kitu leo jua kuna siku ukweli utajulikana. Kwenye CV watu mnajijazia mavitu kibao ambayo sio ya kweli ili uwashawishi Saa ipo nayo saa yaja mfuniko wako utaondolewa na utajulikana.

Aheri ya nyie ambao mmeshaoa na kuolewa hahahaha kwa sisi ambao ni Living Single changamoto bado ni nyingi na kubwa kubwa, unakuata Jambazi anajifoji anakuwa kama Sister wa kanisa Katoliki, Professional Cheater anajifoji kama Baba Mchungaji, kila mtu ajifoji huku makucha yamefunikwa. Unadhani umepata huku ndani kwa ndani mtu anajijua kabisa hili ni bomu ambalo litalipuka saa yoyote. Watu siku hizi wanapendwa kwa vitu vyao na sio kama walivyo, kuna watu wanampenda Papaa sababu ni Creative, Kuna watu wanampenda Mussa sababu anaongea Mapoint, Kuna watu wanampenda Daisy sababu she is very open, wengine wanampenda Clara kwa vile alivyo, kuna wengine wanampenda Prosper kutokana na Macho yake kila mtu anamtazamo wake katika mstakabari wa mapenzi. Unapoingia katika mahusiano ndipo unagundua hawa watu sivyo walivyo, unatumia miaka 3 kusoma mtu ambaye tabia zake ni kama maandishi ya Kiarabu ama Kichina kila unapodhani Kichina kumbe ni Kiarabu, mwisho wa siku mabomu mawili yanaamua kujilipua. Kwanini tusiwe wakweli?Biblia inasema ‘Kama Msingi Ukiharibika, Mwenye Haki atafanya Nini?tusizibe mashimo ya panya kwa vipande vya mikate. Just be open and straight kwenye kile unachokitaka na usichokitaka.
Hakuna jambo baya tena la fedheha mtu uliyekuwa unahesabika decent na una integrity yako kumbe sio ulivyo. Leo hii tukasikia Harry ile gari kumbe alimdhurumu mtu hahaha au tukasikia Addo ameshtakiwa kwa kutoa Rushwa, ama tusikie Josephine anatembea na boss wake, yaani kila ukichangia point hapa kwenye jukwaa watu watakuwa wanaongea yao moyoni. Inakuchukua dakika moja kudanganya watu zaidi ya 100 ila inakuchukua miaka kadhaa watu wale wale kukuamini tena kama walikubaini sivyo ulivyo. Ukibambwa unapoteza ujasiri, ukibambwa unahisi kila siku watu wanakuongelea wewe issue yako. Kwanini Usiwe huru?Kila unapotaka kudanganya chochote na popote just remember hiki ni kipande cha Mkate kwenye shimo la Panya. Jana nimesoma kichekesho kimoja Mchungaji alimpa rushwa Traffic, baada ya siku 2 mke wa traiffic akawa mgonjwa, mkewe akamwomba mumewe ampigie simu mchungaji wao aje amuombee, kwa kuwa baba hakuwa ameokoka alikuwa hamfahamu mchungaji wa mkewe anafananaje. Mara baadaya kuelekezana kwa simu mchungaji akawasili nyumbani kwa ile familia kufungua mlango Traffic anakutana uso kwa uso na Mchungaji, teh teh pata picha unaombaje sasa kwa mgonjwa. Hahaha inakuwa vipi changudoa uliyetembea nae jana usiku anakukuta unahubiri kanisani na mkakumbukana..hahahaha Kama wewe ni A kuwa A.

Nimalize kwa kusema kuna gharama kubwa ya kulipa kwa yale ambayo leo tunayafunika ili tuonekane ndivyo kumbe sivyo. Usifunike Kipande cha Mkate kwenye shimo la panya.


....//Papaa
http://www.samsasali.blogspot.com/

No comments: