Tuesday, August 31, 2010

Papaa On Tuesday Kama Haipo Haipo Tu!Ila Sio Rahisi Kuipotezea


Marafiki Huru hope tuko pouwa, Mara nyingi tumezoea ule msemo wa “Kama Ipo Ipo Tu” yaani kwa maana ya kwamba kama kitu ni cha kwako ni cha kwako hata ikiwaje, lakini tumesahau kabisa kuwa kuna wakati mwingine haipo na haipo kweli lakini tunahitaji hicho kitu ama mtu kwenye maisha yetu ya kila siku. Ukweli unabaki kuwa ipo lakini hatuwezi kuipata na tunahitaji iwe yetu huwezi ipotezea wakati mwingine tunajifarii kama ipo ipo lakini ukweli hiyo tunayoikosa inatuuma na sio rahisi kuipotezea kana kwamba ulikuwa huitaki.

Kuna watu tumetamani sana wawe wenzi wetu kwenye maisha na wengine walifanyika marafiki wazuri sana lakini ghafla mambo yakageuka yakawa ndivyo sivyo je unapotezea?kwa kusema kama ipo ipo?kuna wakati haipo na tunaihitaji kwa wakati huo. Tukiwa chuo nilimpendaga sana yule dada aliyekuwa nyuma mwaka mmoja, Protace aliyekuwa rafiki yangu anakumbuka sana mahusiano yangu na yule dada, wazee wa fellowship akina Rapha, Tangi J, david, Msegu, Mbarikiwa na Sebene group lote walikuwa wameanza mchukulia mama mtumishi, hahahaha Addo pamoja na Tumaini ndo waliokuja kuniambia Papaa umeingia ndiko siko kwa issue moja mbili tatu, baada ya ufuatiliaji wa issue moja mbili tatu nikabaini nimeingia choo cha kike ukweli unaachilia huku bado unahitaji unapetezea wakati bado inakuuma? Then unajifariji kama ipo ipo tu lakini kuna wakati haipo na tunaihitaji kwenye maisha. Ukikaa mbele za watu kana kwamba umeachia na unapotezea ukikaa mwenyewe just alone unagundua kama haipo kweli haipo lakini kupotezea sio rahisi.

Kuna wakati tunatamani tuhame katika ofisi tunazofanyia kazi kutokana na manyanyaso mbali mbali mengine toka kwa waajiri wetu na wengine wafanyakazi wenzetu, umewahi takwa na bosi wako??kama hujawahi usiombe zahama hiyo ikukute, kuna wakati unaumiaaaaaa, kuna wakati unaliaaaaaaa, lakini huwezi ondoka ukasema kama ipo ipo tu why?unajua kamabisa ikiwa haipo huwezi ipotezea bwana pamoja na shida lakini ndo ndo ndo si chururu. Kuna wakati tunatamani wengine kutoka kwenye relationship tulizoingia lakini kweli utoke kwa jeuri ya Kama ipo ipo?thubutuuuuuu, ikiwa haipo huwezi potezeakuwa sawa na ikiwepo. Inawezekana haijawahi kukuta tatizo kubwa kwenye maisha yako ndo maana unaongea kama utakavyo, umewahi waza siku unapofanyia kazi ukiambiwa kuwa kuanzia leo hauna kazi tena utaondoka na kuwaambia watu kama ipo ipo?lakini ukikaa mwenyewe chumbani huwezi ipotezea kuwa eti ipo unagundua kuwa ikiwa haipo huwezi jifanya ipo bado unaihitajikwa kiasi kikubwa tu kwenye maisha. Umewahi waza mchumba wako ama mpenzio siku akifa ama amkiachana kwa namna yoyote ile utajipa moyo kuwa kama ipo ipo?unaweza ukawa unajipa moyo kwenye macho ya watu but still huwezi kuvumilia moyo unaumaaaaaaaaa, kwa sisi tulio wahi experience kukataliwa katika ku-approach tunafahamu namna ambavyo sio rahisi kupotezea moyoni kuna mchakato mahususi “to let it go”. Sio rahisi kupokea taarifa ya mkeo ana ujauzito wa rafiki yako, rafiki yako unayefanya nae biashara amekula capital ya biashara baada ya kumwamini na kumpa then ukasema kama ipo ipo ...kuna wakati tunaikosa wakati tunaihitaji iwepo.
Jiulize mambo mangapi mpaka sasa yamekuwa yakikutesa wewe mwenyewe kwa kujifanya unapotezea eti kama ipo ipo lakini ukikaa mwenyewe na ukikumbuka kichwa kinazunguka na kukuuma mpaka unatamani kulia ama wengine hata kufa, ukikumbuka fedha ulizopoteza, ukikumbuka muda uliopoteza, ukikumbuka ulivyojiotolea kwa kiasi kikubwa...watu wakikuona unasema kama ipo ipo tu...but kumbuka umeshindwa ipotezea kwa sababu ukweli wa moyo kama haipo huwezi ipotezea kimya tu.

Kama ipo Ipo tu! Lakini kama Haipo Sio Rahisi Kuipotezea.

Think Differently and Make a Difference.


…//Papaa

T- SHIRT ZA MARAFIKI HURU

Zile  T-SHIRT  Marafiki huru Bado zipo.weka Oda yako kwa ajili ya Event Ya Marafiki huru ziku ya IDD PILI mfano wa Tshirt Hizo ni huu hapa.hii picha ilipigwa kutoka kwa Rafiki huru alikuwa ameivaa kwenye moja ya Events

Monday, August 30, 2010

Think Differently,Make a Difference



“Think Differently, Make a Difference” Tunaamini Marafiki Huru tuna mawazo Mbadala kwenye Taifa letu, Makanisani Mwetu, Maofisini mwetu, kwenye Familia Zetu hasa katika Jamii inayotuzunguka. We Think Differently and we Make Differences.
Ndo maana tunaamini tunaweza kujenga shule kupitia Watanzania, Tunaamini tunaweza kujenga visima kupitia Watanzania, Tunaamini Maendeleo ya Watanzania yanaletwa na Watanzania na Si vinginevyo. Kwa kushirikiana na Serikali na Kanisa tunabainisha Fursa zilizopo kwenye Taifa letu. We believe Together We Can. Think differently and Make a Difference.
..//Papaa

Sam Sasali a.k.a Papaa: Hillsong - Everyday

Sam Sasali a.k.a Papaa: Hillsong - Everyday: "Papaa Sebene"

Saturday, August 28, 2010

UNAFIKIRI UNA KAZI MBAYA?

Kiponzo kutoka kwa Rafiki huru ADDO

MH MTETEZI WETU YU HAI BY SHUSHO

MH NDANI YA ALL NATION CLUB INT PICNIC 2010

Rafiki huru Emmanuel kawedi akiwa ndani ya all nation club int picnic 2010

MH WALIPOTEMBELEA KAMBI YA WAKOMA KIGAMBONI

Hapa Marafiki Huru walisimamisha Magari kwa ajili ya kupumzika kabla hawajafika Nunge kwenye Kituo walichoenda kutoa misaada, mwenye vuvuzela ni Mratibu wa Safari Protace, Mdada mwenye Suruali ya Kaki ni Anna, Mke wa Protace, Next ni Joseph, then Irene Lyatuu, kwa nyuma mwenye Tshirt Nyekundu ni Clara na mwisho ni Dorcas
Hii ni timu nzima ya Marafiki Huru waliokwenda Kwenye Kambi Ya Wazee na Wenye Ukoma KUle Nunge, Mwombeki anaonekana akijipunguzia urefu uwe kama wa Papaa ili asije akakosewa kupigwa picha kama mpigaji angepiga sinze Ya Papaa, hivi ni baaadhi ya vitu Marafiki Huru walivyovipeleka Kigamboni
Hapa Marafiki Huru wakiwa na watoto walio katika Kambi hiyo Huko Nunge


CHAKULA CHA PAMOJA

Papaa akiwa na Weda pamoja na Anna Protace


MH WAKIWA BEACH

Mara baada ya Marafiki Huru kutoka kwenye kambi Ya Nunge wakaelekea Beach kwa ajili ya Chakula Cha Mchana, hii group walikuwa wanajiita Chipsi Huru, kutoka kushoto ni Protace, Harry,Eliza,Doric,Marcee,Clara,Miembe na Mwombeki
Mwenye Tshirt ya rangi ya Orange ni Rafiki Huru Hudson Kamoga, mwenye mpira ni Irene Lyatuu, kwa nyuma ni Easter na Milembe hapa marafiki huru wakicheza mpira wa Miguu Baharini...Its was awesome mtu wangu
Hawa walikuwa wanajiita Next Level wakati Marafiki Huru walipokuwa wakifanya games huko beach Kigamboni, Kushoto ni Irene, mwenye kuonekana kwa nyuma ni Abigaili, aliyezibwa ni alan, mwenye shati nyeupe ni Nelson, kisha Blandina, Anna na wa mbele ni kiongozi wao Edna

KUMBUKUMBU ZA HARUSI ZA MARAFIKI HURU

Raphael akiwa amepozi na mke Angel siku ya Harusi yao
Rafiki huru Tumaini akiwa amepozi na mkewe Glory
Rafiki huru  Addo Siku ya harusi yake Mjini Iringa
Rafiki huru Godlove akiwa na mkewe Tildalove  siku ya harusi yao

Marafiki huru ndani ya kituo cha yatima-Arusha

Marafiki huru wakipokea maelezo kutoka kwa Mlezi wa kituo

Marafiki huru wakiwasili kituo cha watoto yatima ya samaritan Arusha

Marafiki  huru God,Tumaini,Frank na Raphael wakipata chai kabla ya kwenda kwenye kituo cha watoto yatima


Rafiki huru Neema akiw na Mtoto yatima Jeremiah wa samaritan orphanage centre Arusha
Rafiki huru  Frank  Nsangarufu





SIKU YA MARAFIKI HURU DAR

Musa,Mombeki,Adrew na Mwakibuti wakicheza game siku ya marafiki huru

 Rafiki huru Tumaini akiwa na Ashura

  Baadhi ya marafiki huru wakiwa pamoja