Thursday, January 27, 2011

KUISHI MAISHA YA IMANI KATIKA ULIMWENGU USIOAMINI

KUISHI MAISHA YA IMANI MAANA YAKE NINI

Kuishi maisha ya imani maana yake ni kuwa, kwa kipindi chote cha maisha yetu hapa duniani, kwa kipindi chote cha uhai wetu, na kwa namna yoyote ile inayoashiria maisha kama kuongea kwetu, kutenda kwetu, kuwaza kwetu, kuenenda kwetu, kuvaa kwetu, kula kwetu, kuona kwetu, kukiri kwetu, kutoa na kupokea kwetu, kufanya kazi kwetu, kupigana kwetu, kushinda kwetu, kuomba kwetu na hata namna yote ile ya kuwajibika kwetu kwa watu wengine, tunayafanya haya yote kwa imani. Tunayafanya haya yote kwa uhakika kabisa, kwa kutokuwa na mashaka wala hofu, tunayafanya kama vile tumejua mwisho wake hata kama hatujayaona kwa macho yetu bado. Kama kuna mambo tunatarajia katika kuishi kwetu, basi kuishi kwa imani katika hayo tunayoyatarajia ni kuishi tukiwa na uhakika wa udhihirisho ya kuwa hayo mambo yatatokea na kufanyika halisi maishani mwetu bila kujali changamoto zitokanazo na imani yetu katika mambo hayo.

Katika tafsiri ya kitabu cha Waebrania 11:1, “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”. Kwa lugha nyingine naweza kusema, imani ni udhihirisho wa mambo ninayoyatarajia kuyapata, mambo ninayotumaini kuyapata, mambo ninayotamani na kuwa na shauku nayo katika maisha yangu. Kwa hiyo naishi kwa namna inayodhihirisha na kuthibitisha kabisa kuwa kuna mambo ninayoyangojea hapo mbele. Kama imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, hii inamaanisha kuwa ni muhimu sana kuyajua hayo mambo yatarajiwayo ni mambo gani kwasababu siwezi kuwa na imani na kitu nisichokijua. Kwa mfano, siwezi kuwa na imani kama Yesu Kristo atarudi tena wakati simjui Yesu mwenyewe wala jambo lolote kuhusu yeye, siwezi kusema nina imani Yesu ataniponya wakati hata sijawahi kusikia habari za Yesu na kwamba yeye ana uwezo wa kuponya. Hivyo ni lazima niwe nimesikia habari za jambo Fulani, ni lazima niwe nimeyajua hayo mambo ninayoyatarajia ili niseme sasa nina imani nayo kwamba yatatokea kwangu.

Ninachosema hapa ni hiki, kwasababu imani chanzo chake ni kusikia, ni muhimu sana kujua unasikia juu ya nini. Kila mtu hujenga imani ya kile anachokisikia na zaidi sana kile achokifahamu na kukijua. Ukisikia sana habari za waganga basi utajenga imani yako kwa waganga lakini kitu cha kujua hapa ni kuwa kama wewe ni raia wa ufalme wa Mungu basi ni lazima imani yako iwe katika mambo yatokanayo na ufalme huo. Neno la Kristo ndio msingi wa kujenga imani ya kweli kwa kila aaminiye kwa moyo wake na kukiri kwa kinywa chake kwamba Yesu ni Bwana. Kwa hiyo kama nimeamua kuishi maisha ya imani ndani ya Yesu, ni lazima nizidi kumsikia sana Yesu ili nizidi sana kujenga imani yangu kwake kwenye mambo ninayotarajia. Kabla sijajua kuwa Yesu ni mwokozi nilimdharau na kuwakejeli wote walionambia habari zake, kwa hiyo nisingeweza kuishi maisha ya imani wakati huo. Nilipomjua Yesu ni nani, kwa kusikia, nikajenga imani yangu na kuanza kutarajia mambo kadha wa kadha yaliyondani yake yeye. Kwa hiyo hakika ya mambo yatarajiwayo inakuja kwa kuzidi sana kuongeza ufahamu katika kuyajua hayo mambo yaliyofungwa ndani yake yeye ninayemwamini.

Mambo yatarajiwayo, kwa tafsiri niliyoiweka hapo juu, inamaanisha mambo ninayotumaninia ndani ya imani yangu katika Kristo na haya mambo ni kama:
• Uzima
• Uponyaji
• Baraka za mwilini na za rohoni
• Mafanikio na maendeleo
• Maisha ya ushindi
• Ulinzi
• Uzima wa milele
• Masomo
• Chakula
• Mavazi
• Nguvu

Kwa kuchukua mfano mmoja hapo juu, mimi nimeokoka ingawa nimekuwa naishi maisha ya hali ya chini kiasi kwamba hata mahitaji ya msingi kama chakula, mavazi na hata mahali pa kulala sina, kuishi maisha ya imani katika hali hii ni kuwa na hakika juu ya hayo mambo ninayoyahitaji kuwa nitayapata kutegemeana na imani yangu katika yeye ninayeamini, yaani Kristo, kuwa anaweza kunipa hayo yote sawa sawa nay ale ninayoyafahamu na kuyajua, yale niliyoyasikia amesema kuwa atanifanyia. Ingawa mwili wangu utaonekana kuchakaa lakini imani yangu inanipa nguvu na tumanini kwani ninajua kabisa kuwa ipo siku Yule ninayemwamini atayabadilisha maisha yangu kwa kadri ya imani yangu, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yangu na zaidi sana kwa kadri ya utajiri wa utukufu wake.

Kwa upande mwingine, kuna mambo yasioonekana ambayo nayo tunatakiwa tuishi kana kwamba tumeyaona na hapa Neno la Mungu linasema, imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Neno bayana ni sawa na kusema halisia, imani ni uhalisia, waziwazi au inayooneka kabisa kwa macho ya nyama na damu. Umesubiria mtoto kwa muda mrefu, imani inakupa nguvu na tumaini la kuendelea kuishi maisha yako kila siku kama mama aliyepata mtoto tayari. Bayana. Halisia. Inayoonekana. Kama kuna jambo lolote lile ninalolingojea nab ado sijaliona, ninatakiwa niwe na lingojea kama vile nimeshaliona kama vile Babu Ibrahimu, habari zake zinasema alitarajia yasioweza kutarajia, alitarajia mambo yasiyoonekana kana kwamba yameonekana, alimtarajia Isaka wakati hali yake na nay a Bibi Sara haikuwa na uwezo wa kuwapa mtoto lakini yeye alisubiri katika kutarajia kwake mambo yasiyoweza kutarajiwa kabisa. Nguvu ya imani yake aliipata kwa kumjua anayemwamini.

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani na ndivyo mema yatakavokujia, ndivyo utakavyozidi kupata ushindi maishani mwako, ndivyo utakavyozidi kushinda vita na makwazo ya duniani hapa na ndivyo utakavyozidi kuishi maisha yenye utulivu na usalama kwa maana unamjua yeye akupaye nguvu za hata kupata utajiri. Kwa hiyo kuishi maisha ya imani ni katika hali zote kwa maana pasipo hiyo imani haiwezekani kabisa kumpendeza Mungu kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima, sio ombi, lazima aamni (awe na hakika wa mambo anayotarajia toka kwake) kwamba yeye Mungu yuko na zaidi ya hayo huwapa thawabu, huwapa Baraka, huwapa mambo mema, huwapa mafanikio, huwapa hazina njema wale wote wanaomtafuta. Katika hali zote, kufanikiwa au kutokufanikiwa, kupata au kukosa, raha au mateso imani inahitajika na hivyo wakati wa Furaha wewe furahi kwa imani na wakati wa majaribu ya imani yako usiseme hii sio imani kwani ni vema kuhesabu ya kuwa ni Furaha tupu tunapoingia katika majaribu mbali mbali tukijua kuwa kujaribiwa kwa imani yetu huleta saburi maishani mwetu. Kwa hiyo neno imani lina maneno matano ambayo ni:
1. Hakika-kutokuwa na shaka wala hafu, thabiti
2. Mambo-ahadi za Mungu unazozijua kama Neno lake linavyosema
3. Yatarajiwayo-tumaini la kungojea na kusubiri
4. Bayana-halisia, inayoonekana
5. Yasiyoonekana-kwa macho ya nyama na damu
Kwa hiyo, ninapomalizia ukurasa huu, napenda kusema kuwa kuishi maisha ya imani ni kuishi maisha tegemezi katika kile anachokisema Mungu. Ni kuishi maisha ya mtu wa haki, mwenye haki anaishi kwa imani, anaishi kwa kuwa na ujasiri na uhakika wa mambo yote anayoyatarajia hata kama hajayaona kwa macho yake. Tunawaza kwa imani, tunaongea kwa imani, tunakula kwa imani, tunatembea kwa imani, tunafanya kazi kwa imani, tunaomba kwa imani, tunaangalia kwa imani, tunaenenda kwa imani na kwa ujumla wake yote tunayoyafanya iwe ni kwa neno au kwa tendo tunayafanya yote kwa imani katika jina la Yesu tukizidi sana kumshukuru Mungu Baba.

Kwa maana tunajua ya kuwa pasipo imani, haiwezekani kumpendeza Mungu kwani sisi kama wenye haki imetupasa kuishi kwa imani. Kuna uhusiano kati ya kuwa mwenye haki na kuishi maisha ya imani na haiwezekani mtu akaishi kwa imani bila kuhesabiwa haki katika Yesu Kristo aliye mwanzilishi wa imani yetu. Na huu uhusiano ndio tutakao uchambua na kujifunza juu ya kwa nini mwenye haki aishi kwa imani. Umebarikiwa katika jina la Yesu Kristo!

Thursday, December 23, 2010

UMECHAGULIWA JINSI ULIVYO,JIKUBALI

UMECHAGULIWA JINSI ULIVYO, JIKUBALI HIVYO

1 Wakorintho 1:18-31
“18Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19Kwa maana imeandikwa: “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima na kuzibatilisha akili za wenye akili.” 20Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa umpumbavu? 21Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua Yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale waaminio kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. 22Wayahudi wanataka miujiza na Wayunani wanatafuta hekima, 23lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulibiwa, ambaye kwa Wayahudi ni kitu cha kukwaza na kwa Wayunani ni upuzi. 24Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, yaani, Wayahudi na Wayunani, Kristo ni nguvu na hekima ya Mungu. 25Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu. 26Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi waliokuwa na nguvu, si wengi waliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. 27Lakini Mungu alichagua vitu vipumbavu vya ulimwenguni ili aviaibishe vyenye hekima, Mungu alichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili aviaibishe vyenye nguvu. 28Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, 29ili mtu ye yote asijisifu mbele za Mungu. 30Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi, 31ili kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”

1. Kuchaguliwa maana yake nini-
Mpendwa wangu, napenda nikwambie haya maneno yaliyo katika kichwa cha ujumbe huu kwa mara nyingine tena baada ya kuyasoma hapo juu, umechaguliwa jinsi ulivyo kazi yako kubwa ni kujikubali jinsi ulivyochaguliwa. Nimechaguliwa jinsi nilivyo na ninajikubali hivyo pia na napenda wote mnaosoma hapa mjue kuwa tumechaguliwa jinsi tulivyo na ni muhimu kujikubali jinsi tulivyo. Kabla sijafika mbali napenda kusema maana ya haya maneno ili tunapoendelea tuwe katika kiwango kimoja cha uelewa, shauku yangu ni kuona haya maneno yanakuvusha kwenda hatua na kiwango cha juu, kile kiwango alichokusudia Mungu mwenyewe,kiwango cha wewe kujijua na hata kufika mahali ukajivunia kuwa jinsi ulivyo. Kiwango cha kukupa nguvu ya ushindi ujapopita katika kudharauliwa, kukataliwa, kutengwa, kubezwa, kusimangwa na hata kuabishwa. Amin nakwambia ukijua siri hii, utavuka na kushinda mengi sana yanayoletwa kwako kukuletea dhihaka. Na neema ya Mungu ipo kukusaidia kuelewa katika jina la Yesu. Wengi wamepotea kwa kukosa ufahamu sahihi wa wao ni akina nani na wanatakiwa waishi maisha ya namna gani mpaka wakajikuta wananunuliwa kwa vitu dhaifu na vinyonge sana. Kwa hiyo nataka kwanza nikazie kusema umechaguliwa jinsi ulivyo, umechaguliwa na udhaifu wako na uwezzo wako. Kuchaguliwa ni kuchaguliwa tu.

Maneno ya msingi hapa ni umechaguliwa na jikubali na haya ndo yamejenga msingi wa yote yaliyo humu ndani ya maandishi haya. Najua kuwa wote tunaelewa maana ya neno umechaguliwa au chagua au kuchaguliwa, yote mzizi wake ni neno chagua. Chagua au kuchagua ni kufanya maamuzi ya jambo lolote kutegemeana na hali ya mtu mwenyewe, kwa mfano mimi nikikuchagua wewe kuwa rafiki yangu maana yake nimeamua kukufanya rafiki bila kujali mtizamo wa mtu yeyote wa nje. Hapo nakuwa nimeangalia hali yangu ya ndani na vitu kama upendo wangu kwako na mambo ambayo yananivutia mimi binafsi. Hivyo uchaguzi ni jambo la binafsi sana, kwahiyo mimi nikikuchagua hata kama utasikia maneno yasiyoendana na uchaguzi wangu kwako,hayo maneno hayabadilishi ukweli wa kwamba mimi nimekuchagua. Kwa lugha nyingine ukichaguliwa na mtu,hakuna mtu anayeweza kuja kubadilisha kuchaguliwa kwako. Watu pekee wanaoweza kubadilisha huo uchaguzi ni wewe na aliyekuchagua, kama aliyekuchagua amesema amekuchagua basi hiyo itaendelea hivyo milele ingawa uliyechaguliwa unaweza kukataa na kutokukubali kuwa umechaguliwa.

Ujinga ndo jambo kubwa sana linalopelekea mtu kuishi kama kichaa, bora hata kichaa maaana anajua anatakiwa apitepite mitaa ya majalalani ili apate chakula. Ni muhimu kujua huu msingi mpendwa wangu. Kutokujua mambo na kutotaka kujifunza kujua kumewafanya wengi wajiharibu matumizi yao. Ukichaguliwa umechaguliwa, lakini unaweza ukachaguliwa bila kujua ambayo haitazaa matunda sana. Kumbe msingi mwingine wa kuchaguliwa ni kujua umechaguliwa. Kuna utofauti kama nikikuchagua bila kukwambia na kama nikikuchagua na nikakwambia. Kujua kwamba nimekuchagua kuna nguvu zaidi ya kutokujua.Kuchagua jambo ni maamuzi ya mtu binafsi,na ndio maana wengi waliochaguliwa vitu mbali mbali wanayo mengi ya kusema kuhusiana na mambo waliyokutana nayo. Wengi huogopa kufanya maamuzi ya kuchagua kwa sababu hawataki kuwajibika kwa maamuzi yao bila kujua kuwa kuwajibika ndio raha ya kufanya maamuzi. Mfungwa aliyezoea kukaa jela, anaweza akagoma kuja kuishi uraiani kwa sababu ameshazoea kula kilaini na hataki tena kuwajibika na kufanya kazi halali, utumwa ni mbaya ndugu. Kwa hiyo hiyo ndo mtizamo wangu wa neno umechaguliwa lakini nataka twende hatua ya ndani zaidi hapa.

Siku moja nikiwa kanisani niliwahi kumuuliza mwana wa Mungu mmoja juu ya habari ya Marafiki na nikamuuliza nani ni rafiki yake wa dhati au best friend, akanitajia jina la msichana ambaye wamekuwa nae wote mara nyingi na mpaka watu wanaona kuwa wao ni Marafiki wa kweli. Nikamuuliza kama rafiki yake huyo anajua kama yeye ndiye best friend kwake akasema hana uhakika lakini hivyo ndivyo ilivyo. Nikaendelea na uchunguzi, wakati mwingine nikamwita Yule rafiki aliyetajwa kuwa ndo best naye nikamuuliza rafiki yake wa karibu. Huyu cha ajabu akanitajia jina la rafiki mwininge kabisa na wala sio Yule aliyemtaja. Siku nyngine nikamuuliza Yule wa kwanza utajisikiaje kuwa rafiki unaesema ndio best hajuia kama wewe ndiye best na yeye ana rafiki yake best mwingine? Akasema atajisikia vibaya sana. Inauma sana, kuchagua au kuchaguliwa bila kujua. Pamoja na kwamba unaweza ukawa umechaguliwa bila kujua hiyo haibadilishi ukweli kwamba umechaguliwa maana kama ni maamuzi yameshafanyika.

2. Fahamu kuwa umechaguliwa-Yohana 15:16

“Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi;”
Je, unafahamu au unajua kuwa wewe umechaguliwa? Swali litakalofuata hapo ni je, umechaguliwa na nani? Narudia tena kuwa mpendwa wangu umechaguliwa jinsi ulivyo, jikubali jinsi ulivyo na hakuna namna unaweza kupingana na huu ukweli zaidi sana wote wanaopingana na ukweli huu hali zao hazina matumini sana. Kwa vijana hali ni mbaya zaidi kwa maana kutojua wao ni akina nani kumewafanya waishi maisha ya kuigiza, maisha ya kuangalia video na sinema na kisha kufanya kama walivyoona au walivyosikia. Ukiona mtu yeyote anaishi maisha yasiyo halisi, tambua kuwa yuko kwenye hali ngumu sana ya kutokufahamu haya mambo. Kuishi maisha ya kuigiza ni ishara ya wazi kabisa ya kutojijua wewe ni nani, ni ishara ya kuonyesha kuwa huna thamani na wala huna jambo lolote jema linaloweza kuwafaa wengine kwa hiyo unaamua kuishi maisha ya kuigiza (Copy and Paste Lifestyle). Misha haya ya CPL ni maisha magumu sana maana ni maisha ya utumwa wa maamuzi ambayo yataendelea kuwepo mpaka mtu atakaporudi kwenye msingi wa chanzo chake na kutaka kujua zaidi juu ya yeye ni nani.

Kuna utofauti mkubwa sana kati ya kujua na au kutokujua kuwa umechaguliwa, ni sawa na kusema kuna faida ambazo zinaambatana na kujua na pia kuna hasara za kutokujua, hii ni kwenye jambo lolote katika maisha yako. Ukiwa umezaliwa na humjui baba yako ni tofauti sana na kama siku ile unapojua kuwa Fulani ni baba yako. Watu wengi na hasa vijana wanaishi katika kutokujua mambo mengi sana yanyowazunguka na ndio maana wengi ni mawindo ya ibilisi kwa kutumia vyombo vya habari na Marafiki. Nataka ufahamu kuwa Mungu ndiye amekuchagua kupitia mwanawe Yesu Kristo, kwa hiyo fahamu umechaguliwa. Wengine wanafahamu wamechaguliwa na watu mbali mbali, wengine na dunia na starehe zake, wengine wamechaguliwa na nguvu za giza na mapepo na ni waaminifu sana kutumikia uchaguzi huo. Ninachotaka ufahamu hapa ni kwamba umechaguliwa ingawa kufahamu tu kuwa umechaguliwa haitoshi, ni muhimu kwenda hatua nyiningine ya kumfahamu aliye kuchagua. Je, unamjua aliyekuchagua?


3. Mfahamu aliyekuchagua
Unakumbuka ule mfano wa mwanzo? Ngoja niurudia hapa ili unielewe zaidi. Siku moja nikiwa kanisani niliwahi kumuuliza mwana wa Mungu mmoja juu ya habari ya Marafiki na nikamuuliza nani ni rafiki yake wa dhati au best friend, akanitajia jina la msichana ambaye wamekuwa nae wote mara nyingi na mpaka watu wanaona kuwa wao ni Marafiki wa kweli. Nikamuuliza kama rafiki yake huyo anajua kama yeye ndiye best friend kwake akasema hana uhakika lakini hivyo ndivyo ilivyo. Nikaendelea na uchunguzi, wakati mwingine nikamwita Yule rafiki aliyetajwa kuwa ndo best naye nikamuuliza rafiki yake wa karibu. Huyu cha ajabu akanitajia jina la rafiki mwininge kabisa na wala sio Yule aliyemtaja. Siku nyngine nikamuuliza Yule wa kwanza utajisikiaje kuwa rafiki unaesema ndio best hajuia kama wewe ndiye best na yeye ana rafiki yake best mwingine? Akasema atajisikia vibaya sana. Inauma sana, kuchagua au kuchaguliwa bila kujua.

Hili swali ni muhimu sana, umechaguliwa na nani na kwanini? Ni muhimu kujua umechaguliwa na nani maana maisha yetu hapa duniani ni maisha ya kuchagua. Sisi wenyewe tunavitu vingi tulivyochagua wenyewe na sasa hivi hivyo vitu ni mali yetu. Mke anamchagua mume na mume anamchagua mke, anaechagua ana nguvu zaidi ya yule anaechaguliwa. Nini nasema hapa? ukisoma Neno la Mungu utaona linasema waziwazi kuwa sisi tumechaguliwa toka mwanzo na pia kuwa sisi tunampenda Mungu kwasababu yeye ndo aliyeanza kutupenda kwanza. Hamna mtu aliyejichagua mwenyewe kama vile hakuna aliyejiumba mwenyewe. Asili yetu ni Mungu mwenyewe kwa maana alituumba kwa sura yake na mfano wake.

Ukienda dukani kunua nguo au simu ni kitu gani kinakufanya uichague nguo au simu Fulani na kuiacha nyingine wakati ziko nyingi tena za aina mbali mbali? Kitu gani kinakufanya umchague rafiki huyu na kumuacha huyu? Je unajua kuwa uchaguzi unahusisha pande mbili, yaani upande unaochagua na ule unaochaguliwa? Kwa mfano ukienda sokoni kununu nyanya utakuta mafungu kadhaa yamepangwa mezani na kati ya hayo wewe mchaguaji unataka fungu moja. Kwahiyo kwa upande mmoja wewe unachagua fungu la nyanya utalooona linakufaa na kwa upande mwingine hilo fungu la nyanya litawakilishwa na muuzaji kukubaliana nawe kwa misingi ya bei iliyopangwa. Kwahiyo uchaguzi ni maamuzi na kila uchaguzi una gharama zake. Kuna gharama za kuwa na rafiki uliyenae sasa, kama hukulipa mwanzoni mwa urafiki basi unalipa sasa au utalipa baadae, cha msingi ni kuwa ni lazima ulipe gharama ya kufanya maamuzi ya kuchagua.

Yohana 15:16 inasema “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi… “Aliyetufia ndiye aliyetuchagua. Tumechaguliwa na Mungu, aliyeziumba mbingu na nchi, umechaguliwa na Bwana wa majeshi, Mfalme wa utukufu, Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana wote unaowajua na hata wale usiowajua. Tumechaguliwa ndani yake Kristo Yesu, ili tuwe na urithi katika ulimwengu huu na ujao pia, ametuchagua tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. Efeso 1:11.

4. Unajisikiaje kujua umechaguliwa na Mungu

Zaburi 34:8 inasema, “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema, heri mtu Yule anayemtumaini”
Hebu nikuulize swali, ulishawahi kujidharau, kumdharau mtu, kudharauliwa? Ulishawahi kujiona hauna maana na haufai hata kufika mahali ukataka kujiua au kwenda kujificha porini?. Ulishawahi kujilinganisha na rafiki yako,au ulishawahi kutamani kuwa kama rafiki yako,kuvaa mavazi kama yake, simu yake,wazazi wake,mali zake na hata muonekano au haiba yake? Ulishawahi kukataa kufanya jambo Fulani uliloambiwa ulifanye kwa kutojiona wewe huwezi kulifanya? Hapa kuna maswali mengi sana ya kujiuliza na yote yatajibiwa katika waraka huu. Mimi binafsi nimeshapita kwenye vipindi mbalimbali vya maisha kama maswali haya yalivyouliza. Kuna wakati nilijiona nimezaliwa kwenye ukoo duni, familia duni, mkoa duni na hata nikakua kwenye mazingira magumu sana. Pia nimeona watu wengi wengi sana wakishindwa kufanya na hata kutofikia malengo yao katika maisha kwasababu ya kupita katika vipindi mbali mbali sawasawa na maswali hayo hapo juu.

Kadri utakavyokuwa unasoma utaona majibu ya maswali mengi ulonayo moyoni na mpaka ujue ni kwanini watu wengi wanafika mahali wanajiona hawafai na hawana msaada wowote katika jamii. Fahamu kuwa kupita kwenye maisha magumu na yanayokatisha tamaa na kuishia hapo haitoshi, ni lazima uvuke upande wa pili ambao ndio msingi wa yote nitakayoyasema hapa. Watu wengi wamepita katika maisha hayo, wengi wamebaki katika hali hizo na wachache wameenda mpaka upande wa pili. Wengi wamekatishwa tamaa na ndugu na jamaa wa karibu na wamekubali hiyo hali mpaka sasa wanateswa na hiyo hali. Wengi wametukanwa na kutamkiwa maneno magumu juu ya maisha yao kiasi kwamba wanaona hakuna umuhimu wa kuishi. Wengi wamehubiriwa injili ya mapepo, wengi wanajiona wana laana, wana mikosi, wana nuksi kumbe nuski ni ufahamu wao wenyewe.

Ngoja niseme hap akuwa umechaguliwa na Mungu, Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, mwenye nguvu zote. Haujachaguliwa na waziri mkuu, rais, mwalimu mkuu wa shule, kiranja, baba wala mama bali umechaguliwa na Mungu mwenyewe. Unajisikiaje kuchaguliwa na Mungu mwenyewe? Unajisikiaje kujua kuwa Mungu ndiye aliyekuchagua na kwamba hakuna anayeweza kubatilisha uchaguzi wake? Kisiasa watu hukataa matokeo ya uchaguzi na kwenda mahakamani, lakini hao ni wanadamu, nani atakaempinga Mungu kwamba amekuchagua? Yeye ndiye mwenye haki na ufalme wa ke unatangaza Furaha, amani na haki katika Roho Mtakatifu. Warumi 14:17.

5. Aina gani ya vitu au watu vi(wa)mechaguliwa na Mungu
Ukisoma 1 Wakorintho 1:26-29 utapata jibu la moja kwa moja kuhusu aina ya vitu alivyovichagua Mungu. Nitakusaidia kuvitaja hapa na kukuelezea kidogo ili usije uakatafuta sababu ya kubaki na kuishi maisha katika ujinga. Lakini ili unielewe vizuri ngoja nianze kusema vitu au watu ambao Mungu hajavichagua au hajawachagua.
• Si wengi wenye hekima ya mwilini
• Si wengi wenye nguvu
• Si wengi wenye cheo
• Si wengi wenye fedha na utajiri
• Si wengi wenye historia nzuri za maisha yao
• Si wengi wenye sura nzuri na za kuvutia
• Si wengi wenye elimu,

Na listi inaendelea na hawa wote si wengi wao walioitwa ingawa huenda kabisa kuna wachache wao walioitwa. Hapo hebu tujiulize swali, wengi walioitwa ni watu wa namna gani sasa kama hao wote sio wengi walioitwa? Hili swali nalo linajibika vizuri kabisa, biblia inasema Mungu amechagua vitu vifuatavyo:
• Mambo mapumbavu
• Vitu dhaifu
• Vitu vinyonge
• Vitu vilivyodharauliwa
• Vitu ambavyo haviko
• Watu wasiofahamika
• Watu wasiovutia
• Watu wasio na elimu
• Wasiotoka kwenye familia bora

Na hata hapa mlolongo ni mrefu kuutaja, lakini hata kwa mifano unaweza kujifunza, kwa mfano: Musa alitoka wapi, mfalme Daudi je, Nabii Isaya, Yeremia au Daniel? Vipi kuhusu Yesu mwenyewe? Mtoto wa fundi seremala, anachezea mbao, nani alimjua? Vipi kuhusu wewe mwenyewe unaesoma hapa? Kumbuka nyuma kidogo, tangu umezaliwa, ukakua na ukaenda shule ya msingi, secondary mpaka hapo ulipofika ni watu wangapi umewaacha njiani na wengine hata hujui wako wapi, wewe ni nani? Kwanini uchagulliwe na Mungu na una thamani gani? Nilipojua hii siri kwamba Mungu amenichagua na udhaifu wangu, na yote niliyonayo nilianza ukurasa mpya katika maisha yangu.

6. Ufahamu wa Ki-Mungu unakupa kujua thamani yako

Warumi 1:28 inasema, “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.”
Ukiendelea kusoma misitari iliyobakia utashangaa sana. Faida za kukataa kuwa na Mungu katika fahamu za mtu zimetajwa waziwazi nazo ni:
• Kujawa na udhalimu wa kila namna
• Uovu na tama mbaya
• Kujawa na husuda, uuaji, fitina, hadaa
• Kuwa na nia mbaya
• Kusengenya
• Kusingizia
• Kumchukia Mungu
• Kuwa na jeuri
• Kutakabari
• Wenye majivuno
• Kutunga mabaya
• Wasiowatii wazazi wao
• Wasio na Rehema
• Wachochezi

Anything has a price to either pay or receive. When you receive it simply means that you are being bought by and if you are paying it means that you are buying something. Price is how much needed to get something or loose something. Price is both way, receiving and giving. But value determines price-that is how much a book is sold depends completely on the value it carries. Value is determined by various things that have been used to make up something; these are materials used or ingredients or contents. This simply means how scarce or plentiful those materials are, that is how much value the product will have. In most cases, where there is no value there is no price. Value is both internal and external and there is a big difference between having certain values and knowing that you have them. Most of the things that people don’t know their values are priceless or cheap, this applies to everything including people. Knowing how worthy you are will make you in the position to even determine your price.

For example, in labor market where price is given according to merit and other qualifications, you easily know how much to pay someone with a certificate, a diploma, a degree or masters. Here education becomes one of the ingredients that make that job seeker and later his various abilities will be seen and used to promote and motivate. Beyond values and ingredients there is a source or the origin. The source determines everything, the source determine

Basically in our day to day dealings we pay our prices in regards to our choices we make. Economically, this idea is called opportunity cost. So we are sold and sell just as we buy and being bought. If I wake up in the morning and decided not to go to work-then my price is the very reason that made me not to go. If I did not go because of being lazy, then laziness is my price, got it? My value is connected to the vision and mission of God to me. Mission and vision of God is only found only in his heart and in his mind, moreover the heart and mind of God is demonstrated to what he speaks, I mean his word.

Lakini pia wengi wako tayari kununuliwa hata kwa chipsi (viazi vya kukaanga vilivyokatwakatwa), wengi wananunuliwa kwa pesa, mali, magari na vitu vinavyoonekana ni vya thamani sana. Wengi wamewauza ndugu zao kwa mizimu kwa sababu ya utajiri. Huu ni ukosefu wa akili, maarifa na hekima kwa kiwango cha juu sana. Tafsiri ya mambo yote haya ni kuwa, watu wengi hawajui thamani ya maisha yao na thamani yao wenyewe. Hebu jiulize wewe ni wa thamani gani. Ninachotaka kusema ni kuwa, kwa ujumla kuna hali ya kutojiamini, kujidharau, kudharauliwa ambayo ipo katika jamii na hasa ndani ya mwili wa Kristo. Kwa hiyo ni muhimu tukakumbushana tena kuwa, kila mtu amechaguliwa jinsi alivyo na inampasa kujibali hivyo alivyo. Swali la msingi hapa ni hili: Hayo yote yanatoka wapi?

7. Kwanini Mungu amekuchagua wewe
Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi nilyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.”

Nataka ujue hapa kuwa baada ya kujua hayo yote kwamba Mungu amekuchagua, ni muhimu sana kujua sababu au dhumuni au malengo au matarajio ambayo Mungu anayo ya kukuchagua wewe na majibu yake pia yako wazi kabisa kwenye kitabu hiki hiki cha wakorintho. Amekuchagua jinsi ulivyo ili:
• Ili kumzalia Mungu matunda yadumuyo
• Ili utumike kuwaaibisha wanajiona wana hekima
• Ili utumike kuwaaibisha wajionao kuwa wana nguvu
• Ili Mungu avibatilishe vitu vilivyoko kupitia wewe
• Umechaguliwa kwa sababu wewe ni mali yake
• Una chapa yake-sura na mfano wake
• Kwasababu ameamua kukuchagua

Wednesday, September 22, 2010

NAFASI YA MTOTO KATIKA JAMII ISIYOMJALI

Inawezekana kabisa kuwa jamii imechoka hata kusikia habari za watoto, huenda watu wakawa hawako tayari hata kutaka kujua mambo mbalimbali yanayotokea kwa watoto na huenda jamii haina hata mikakati maradufu ya kuhakikisha utetezi wa haki za mtoto ni jambo la muhimu katika majira na nyakati zetu. Nadhani hata katika hatua na ngazi ya kwanza kabisa ya familia, mambo ya mtoto na nafasi yake katika familia si vitu vya kuzingatiwa sana. Hii ni picha ndogo na picha kubwa yake ni ukweli kwamba kama mtoto hajapewa nafasi katika familia atawezaje kupewa nafasi katika jamii kubwa inayomzunguka.
Mtoto anaweza kuwa wa kike au wa kiume, mrefu au mfupi, wa rangi yoyote, kabila lolote, dhehebu au dini yoyote, tajiri au masikini ili mradi tu awe na umri chini ya miaka kumi na nane (kwa tafsiri ya andiko hili). Pengine kwa tafsiri za mashirika mengine mtoto ni chini ya miaka kumi na nne (14) au kwa namna yoyote ile ambayo wewe binafsi na au pamoja na jamii yako mnamtafsiri mtoto kwa namna hiyo. Cha muhimu hapa ni kumzungumzia mtoto kama unavyoelewa na la muhimu zaidi katika makala hii ni Nafasi ya huyo mtoto katika jamii isiyomjali labda tu kama unaona jamii inamjali tena kiasi cha kutosha. Lakini huenda ukaona kama jamii yetu inamjali, sikatai labda tu ni kwa kiasi gain na ukaribu gani wa kumjali na pia hebu tutake kujua neno jamii linamaana gani ndipo tupate kujua kama ni kweli au la kwamba jamii haimjali mtoto.

Ni muhimu kumjua na kumtambua mtoto kwa namna unavyoweza ili kupunguza madhara ambayo watoto wanayapata kwa kutokuwa na ufahamu tu. Kukosa ufahamu ni kubaya na kunaumiza sana maana kinyume chake ni kuwa na ujinga wa kumtosha mtu kiasi cha kutotaka hata kushauriwa. Na alama ya muhimu na huenda ya kwanza kabisa ya mjinga au mpumbavu ni ujasiri wake wa kutotaka kushauriwa, ujasiri wake wa kujiona kuwa hawezi kukosea jambo na huu ni umasikini wa hali ya juu sana. Kuna mambo mengi sana ya kujiuliza juu ya nafasi ya mtoto katika jamii isiyomjali. Kwanza watoto wamekosa watu madhubuti wa kuwatetea na kuwasemea kwa moyo mmoja bila kuingiza matakwa yao binafsi. Hawa watu wapo wachache sana kiasi kwamba wengi zaidi yao wanahitajika na ndio maana mtu kama huyo akifanya jambo lolote ni rahisi tu kujulikana maana ni wachache.
Pili, watu wamekuwa na moyo wa kutojali maana wengi wamejikatia tama ya kuishi au ya kuiona Tanzania mpya. Mimi sio tu kwamba naamini kuwa Tanzania mpya iko njiani inakuja bali pia nina hakika kuwa hilo liko hivyo na si vinginevyo. Tunamiaka michache tu ya kuiona Tanzania iliyojaa taarifa mbalimbali za uovu na ufisadi katika maeneo yote na hata kusikia watoto wadogo kabisa wa miaka chini ya mitano wakibakwa. Muda umekwisha, usiku umeendelea sana na sasa tazama ni mchana mweupe pee. Kama unasoma haya maandishi na umekata tama nakushauri kwa upendo kuwa uwazavyo sio na muombe Mungu akusaidie uishi miaka ishirini ijayo ili uwe shuhuda pamoja na wengi wanaotazamia kuzaliwa kwa taifa la Tanzania. Na njia pekee ya kulizaa taifa jipya la Tanzania ni kuwekeza kusiko na unafiki kwa watoto na vijana wetu.
Tatu mtoto anaunganishwa na taifa moja kwa moja. Sio tu yeye ni taifa la kesho kinadharia bali yeye ndiye kesho yenyewe, yeye ndo msingi, yeye ndo urithi wenyewe, mtoto ndio uthibitisho wa kuwepo kesho yaani kizazi kijacho kinategemea watoto. Unaweza kuwaza kama Mungu akizuia watu kuzaa na kupata watoto itakuwaje? Lugha yake ni rahisi tu, hiyo itamaanisha kuwa Mungu anataka awamalize kabisa wanadamu maana hakuna kizazi kinachoendelea. Usishangae kwanini namtaja sana Mungu maana wengine walio vipofu anaweza tu akakwazika na kuumia kwa sababu namtajataja sana Mungu, sasa unataka nimtaje shetani? Namtaja Mungu kwasasbabu moja kubwa: ndiye ninaye mwamnini na kumtegemea na sio mwingine kwa hiyo sahau kwamba kwa namna yoyote ile nitamtaja shetani au yeyote afananae. Kwa sababu hiyo Mungu anataka tuendelea kuishi na ndo maana ameruhusu vizazi viendelee kuwepo na kuja na hiyo inaonyesha nafasi ya mtoto katika moyo wa Mungu.
Jamii ni mazingira yanoyomzunguka mtoto, ni watu wanaoishi au kuwepo mahali ambapo yeye mtoto yupo kwa wakati huo wa kudumu au wa muda mfupi, kwa mfano jamii ya kwanza kabisa ambayo mtoto anakutana nayo hata kabla hajazaliwa ni mama yake, pale anapokuwa tumboni mwa mama yake. Akizaliwa anakutana na jamii kubwa zaidi ya familia yake na hii ndio hasa hutengeneza mazingira ya makuzi na malezi ya mtoto kwa mara ya kwanza kabla mtoto hajajihusisha na jamii kubwa zaidi. Pia akitoka kwenye familia mtoto anakutana na jamii kubwa zaidi ya marafiki anapokuwa maeneo mbali mbali kama shule, kanisani, michezoni, anapotembea, akiwa kwenye usafiri na hata akiwa kwenye mikusanyiko mbalimbali. Na kwa kadri ya namna mtoto anavyokua ndivyo jamii yake inavyopanuka zaidi na kumfananisha nayo. Hapa tunaweza sasa kusema kabisa kimpangilio mgawanyo wa jamii anayokulia mtoto toka ya kwanza mpaka ya mwisho na hii itatusaidia sana kubaini ni wapi tatizo linaanzia na nini basi kifanyike sasa.
Mgawanyo wa jamii anamokulia mtoto

Kama nilivyoelezea hapo juu utaona na hata ukitaka kuthibitisha hili ninalosema wewe mwenyewe ulishawahi kuwa mtoto na ulipokuwa unakua kuna jamii fulani ulikutanishwa nazo na au ulikutana nazo. Kwahiyo hapa chini nitazipanga jamii hizo kwa mpangilio na pia kutokana na umuhimu wake kwa makuzi na malezi bora ya mtoto.

1. Tumboni mwa Mama

Nafasi ya mtoto kaatika jamii isiyomjali ni swala refu sana na huanzia mahali ambapo watu wengi hawatilii maanani sana, tumboni mwa mama. Hapa mtoto anakuwa katika hali ya mimba na ni rahisi tu kuona kuwa mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake hayuko katika jamii lakini mimi nakwambia tayari anakuwa ni sehemu ya jamii kwani ni kiumbe hai na jamii inakuwa inamsubiria kufika kwake na tena inampigia na mahesabu yake. Kwa maana hii thamani na utu wa mtoto unaanzia tumboni mwa mama, akiwa hata hajazaliwa na hapa duniani kuna watu huwangojea watoto wao kwa hamu kubwa sana na wengine huamua hata kuwaua kwa kutoa mamba.
Mtu yeyote anaehusika katika mchakato wa kutoa mimba (Kiwango cha juu cha uuaji) sio kwamba tu anajisaliti yeye mwenyewe bali anamsaliti Mungu aliyempa uwezo wa kupata mimba, anmsaliti mtoto wake mwenyewe na watoto wengine walio katika hali hiyo ya mimba, anaisaliti jamii inayotarajia kuja kwa rais au waziri mkuu huyo, anafanya usaliti katika mabo yote na hali zote za binadamu. Inahitaji ujasiri wa kishetani kufikia hatua hiyo ya uuaji maana kazi za shetani ni tatu tu, kuua, kuchinja na kuharibu na nisikitiko kuona kwamba mawakala wa shatani wamekuwa wengi kiasi cha kutisha. Maana mawakal hawa wako kila mahali, manyumbani, kanisani, misikitini,mashuleni, makazini,mitaani,serikalini,wako pia Tanzania (na katika mikoa yake yote) na dunia nzima, ni Furaha iliyoje kwa shetani!.
Watu wanaotoa mimba, watu wanaosaidia wengine kutoa mamba, watu wanaoona kuwa kutoa mimba ni suluhisho la matakwa yao kwa wakati huo na mtu yeyote anapigania haki za utoaji mimba sio kwamba tu amekosa ufahamu juu ya mtoto na haki zake bali ni mzigo kwa akili zake mwenye, ni mjinga kwa ufahamu wake mwenyewe na muuaji kwa upumbavu wake mwenyewe. Mtu wa namna hii ni hatari kuishi nae kwani kuua yeye sio swala kubwa sana, unaweza ukalala nae na usiku akaamka akachukua kisu akakuua. Napenda niseme hapa kuwa hakuna sababu yoyote inayofaa au kupendeza ambayo kwayo twaweza kusema ni salama kuua kwa mfumo wa utoaji mamba.

Huu ni upungufu wa maadili, hekima, ufahamu na utu na ndio maana mtoto hana nafasi yoyote kwa maana jamii haimjali. Kama jamii inamjali mtoto haiwezi kuruhusu uuaji katika mfumo wa kutoa mamba maana hata akiwa tumboni anaitwa mtoto na wakifanya vipimo hospitali anaonekana akipumua, akila na tena akiwa wa kike au kiume. Uuaji ni dhambi na kuwa na dhambi ni kuwa na uadui na Mungu na mwisho wake ni jehanamu ya moto na mateso ya milele na hapo haijalishi ni mtoaji mamba, ni aliyemshauri, ni aliyempa pesa kwenda kutoa, ni mvulana aliyekataa kuwa mimba si yake hivyo binti akawa na hasira mpaka akaenda utoa mamba au mtu yeyote yule wa ngazi yeyote ile katika jamii. Sina shaka kwamba wote wanofanya hivyo watalipwa kwa kadri ya wanavyopanda. Namaanisha kuwa hakuna sababu ya kuvutia inayoweza kufanya utoaji mimba uonekane ni jambo jema na kutufaa sana katika jamii yetu, kumbuka kuwa kuwa huru kunaenda na kuwa na nidhamu katika uhuru uliopewa (Freedom is about Discipline and not misbehaviors) kwahiyo usije ukautumia uhuru wako kwa kufanya yasiyo pasa.

Katika hali kama hizi ni nini nafasi ya mtoto katika jamii kama hii isiyomjali, jamii isiyotaka hata kumuona kwa macho na iko tayari kumuua akiwa tumbani mwa mama? Ni ajabu kuona katika jamii hii kwamba watu wameenda kusomea namna nzuri za utoaji mimba, namna nzuri za kuwashauri watu kutoa mimba badala ya kuwashauri namna nzuri za kutopata mimba na kama uwezo wa kupata au kutopata mimba uko mikononi mwao. Mtoto hana nafasi katika jamii hii lakini bado watu wengi na mashirika yasio na yaliyo ya kiserikali yanatengeneza pesa nyingi kwa matumizi yao binafsi kwa kupitia mgongo wa mtoto. Hakika mtalipwa na mimi nitakuwa mmoja wa watakaoshuhudia mnavyolipwa hapahapa duniani. Huu ni ujumbe wenu na tena ni bora usingesoma waraka huu, kwakusoma kwako ndio umetangaza kuwa ni mwisho wa wewe kufanya hayo uliokuwa unafanya. Ukiamua kuendela kuyafanya wewe fanya tu lakini nakuhakikishia kuwa jicho la Bwana Mungu linakutizama na litakufuatilia mpaka utakaporudi kwake au umkatae milele.
Tunawezaje kuwa na ujaisri wa kusema tunawapenda watoto wakati tunakula pesa zao? Tunanunua magari ya kifahali na majumba makubwa kutoka kwenye pesa za watoto, hii ni ajabu sana. Mbona vifo vya watoto vinaongezeka kila siku? Wengi wao wanakufa na malaria, swali langu ni kuwa miradi yote ya kugawa vyandarua na pesa hizo zote zinaenda wapi? Mtanzania mwenzangu ni bora usingesoma waraka huu lakini kama umesoma na ujue tu kuwa ndo mwisho wako wa kufanya hayo uliyokuwa unafanya, amini usiamini. Utalipwa huku watanzania wote tunaona. Ni ajabu sana kuona nchi ya kwetu wenyewe, watoto wa kwetu wenyewe,sisi wenyewe ni wamoja na wazalendo wa nchi yetu leo hii wewe mtanzania unaiba fedha za watoto wa watanzania wenzako tena wale walio masikini kuliko wewe unaenda kujengea nyumba na kuwapeleka watoto wako kwenda kusoma nje, huu ujasiri unaupata wapi? Huu ujasiri hakuna mwanadamu aliyenao ni shatani tu.
Mama mjamzito anatunzwaje kama kweli tunajali kiumbe alichonacho tumboni? Ninyi akina baba mnaowapiga wake zenu wajawazito akili zenu ni zilezile mlizokuwa nazo wakati mnawachumbia? Je, mlipanga kupata watoto? Kama mlipanga mbona unampiga mkeo tena wakati ni mjamzito? Kwanini usingempiga kabla hajawa mjamzito? Hujui mtoto akiwa tumboni mwa mama yake hulia pamoja na mama yake? Ulishawahi kuliona chozi la mtoto akiwa tumboni mwa mama? Unajua atake lifuta hilo chozi? Hakika yako ni bora usingesoma waraka huu. Ni kweli jamii inamjali mtoto?
Wewe mama mjamzito unamlisha mtoto wako tumboni chakula gani? Sasa ndo nashangaa kwamba mama mjamzito anaenda na mtoto wake mpaka kilabuni na anamnywesha pombe, mataputapu huku akifurahia, hivi hujui unachokula wewe na mtoto wako tumboni anakula hicho hicho? Hujui kuwa utaalamu mwingi unapunguza mbao ya maana kuonekana hayana maana wala umuhimu wake? Kwanini unajuta kuipata hiyo mimba? Ni kweli kwamba kujuta kwako kumekufanya umuite mtoto wako Majuto? sasa huu ni utabiri wa kishetani kabisa,kwanini usimwite Baraka? Tafuta kujua watoto wote wenye majina kama Majuto,Shida,nk utaona maisha yao ya leo. Jifunze.

Ni kweli kwamba kila binadamu ana haki ya kuishi? Kwanini anaeua mtu kwa kisu au risasi anapelekwa gerezani na kuchukuliwa hatua kali za kisheria na mtu anaua kwa kutoa mimba anapongezwa kwa tafrija za ushindi wa sababu ya utoaji mimba? Tukia la uuaji likitokea mahali Fulani na vyombo vya dola vikienda sehemu ya tukio mtu yeyote atakae kutwa katika eneo hilo kisheria atashikiliwa na polisi akiisaidia polisi katika uchunguzi,sasa mbona mtu akitoa mimba si yeye wala aliyemtoa mimba,wala aliyempa mimba anashikiliwa kwa kitendo hich cha kinyama? Jamii inamjali kweli mtoto?
Dada zangu inakuwaje mimba upate mwenyewe kwa moyo mweupe, maana unajua kabisa unapofanya mapenzi ni vitu gani kadhaa vyaweza kutokea,halafu unaenda kuua bila hata woga wowote? Huu sio moyo wa mwanadamu. Wewe unazaa mtoto mchanga unamuweka kwenye mifuko tena mifuko ambayo hata serikali imeikataa ndo unaenda kumtupa jalalani,wewe ulitupwa? Kwani ukienda kuomba msaada kwamba jamani mimi sina uwezo wa kulea mtoto huyu nani mwenye utu atakaekataa? Ni nini nafasi ya mtoto katika jamii hii isiyomjali??

Nauliza hivi inakuwaje wewe mvulana unafanya ushirika wa kupata mtoto na binti halafu unaikataa hiyo mimba kwamba sio yako unakuwa unawaza nini? Unajua maana ya wewe kumkataa huyo mtoto? Unadhani utaikimbia hiyo mimba milele? Ulishasikia mtu ameikimbia damu yake? Unajidanganya.
2. Mama na Baba

Mtoto anapozaliwa tu anakukutana na mama yake kwanza. Wakati huu ni wakufurahi sana na kumshukuru Mungu kwa kumleta mwanadamu mwingine ambaye atakuwa mmoja kati ya watu mashuhuri sana nchini na duniani. Ni tukio zuri sana kwa majira haya na hivyo mama anakuwa jamii ya kwanza kabisa ya mtoto kuanza kusikia, kuona na kujifunza kwake. Kitu ambacho unaweza usikijue ni kuwa maneno yote unayoyasema mtoto anasikia. Anaefuata katika kupanua jamii hii ya mtoto ni baba. Mitizamo ya wazazi kwa mtoto anaekua ni ya maana nay a umuhimu wa pekee sana.
Maneno wazazi wanayokiri kwa habari ya mtoto wao ni muhimu maana ndiyo yanajenga msingi wa maisha ya mtoto wao. Ajabu zipo nyingi duniani na moja kati yazo ni kusikia mama au baba akimuita mtoto wake mbwa,Malaya,shoga,nyoka,mende,bwege na hata matusi makubwa ambayo hata mtoto mwenyewe anashangaa kwani ni lugha asiyoifahamu na hajizoea kwa namna hiyo. Matokea yake mtoto anakuwa katika maneno na matusi ya wazazi na hivyo tabia zake zinaendana na yote yaliyosemwa juu yake na wazazi wake.
Mpaka sasa nimeona vitu vya kwanza kabisa ambavyo watoto wengi huanza kusikia na kuona ni mambo yasiyo faa, matusi, picha za ngono, mambo ya ulevi, uzinzi na vitu vifananvyo na hivyo. Imenichukua muda sana mimi kuacha kutukana kwani toka nakua katika jamii ileile iliyokuwa hainijali nilianza kusikia mambo hasi zaidi ya chanya. Nilianza kumjua shetani na mambo yake kuliko Mungu na wema na upendo wake na ndio maana ni rahisi zaidi leo kusema habari mbaya kuliko nzuri. Kama huamini wewe leo nenda ukabake mtoto, uone jinsi dakika tano zinavyoweza kuitaarifu Tanzania na nchi za nje huo ubaya. Lakini ukiandika swala jema na la kuisaidia jamii kama hili utaona watu watakavyosaga meno ingawa kwa hili langu kusaga meno sio jibu, jibu ni mabadiliko ya mitazamo ya maisha na hali tabia.
Nawauliza wazazi,je ni sawa mtoto kuangalia vipindi vyoote katika luninga? Usalama wa mtoto wako uko wapi? Enyi wazazi mbona mnatuua sisi watoto wenu polepole kama vile sisi ni miti? Vipi kuhusu vipindi vya redio? Huu ni utandawazi? Mbona mnatulazimisha kushika imani zenu huku mkitupa uhuru wa mambo yasiyofaa? Sio mimi nashangaa peke yangu bali hata shetani mwenyewe anashangaa kuona baba na mama wanamchukua mtoto wao wanenda wote disco huku wakiielezea hiyo hali kuwa ndo maish ya kisasa. Ukweli ni kwamba sio vitu vyote vinavyofaa japo vyote ni vizuri na vinapendeza sana. Hata siku moja mzazi hajawahi kumsifia mtoto wake zaidi ya kumponda na kumdharirisha usiku kucha kama vile ni vyama vya upinzani. Inafika wakti sasa masikio na macho ya mtoto yanaota sugu na hapo sasa kibao hubadilika na mtoto anaanza kuonekana msumbufu kwa wazazi wakati uhalisia ni kwamba wazazi ndo waliomuandaa kuwa hivyo.
Wewe baba unajisikiaje kufanya ngono na mtoto wako mwenyewe? Ni raha kiasi kwamba huogopi kuwa unaweza kufa hapohapo katika tendo hilo na ukakutwa hapohapo? Hujui palipo na mizoga hapakosi kunguru? Umetumwa na Mganga? Kwanini huyo Mganga asikupe binti yake? Kwanini hutaki kufikiri? Huoni kama upumbavu wako mwenyewe unakumaliza na ujinga wako unakuangamiza? Hiyo ni laana, umelaaniwa wewe ufanyae hayo yote, umelaaniwa.

Utasema nimekutukana, wakati mimi nakusaidia utoke katika upofu wa macho yako na utazame uhalisia wa mambo na uache kufanya mabo kama mnyama. Ni ajabu unamtani mtoto wako? Unamnyemelea mtoto wako anapokuwa bafuni? Una akili kweli wewe? Unaangalia nae picha za ngono wakati mama yuko hospitali anaumwa, wakati mama kasafiri kwenda kumlipia ada ya shule? Baba ndio kichwa cha familia, je hii inamaana ufanye unavyojisikia? Utalipwa nasi tukishuhudia hapahapa duniani, huo moyo na ujasiri haupo kwa mwanadamu awae yote

Vipi mama unapomshauri mtoto wako kuwa mjanja mjini maana yeye anakitega uchumi? Huoni aibu kumuingiza mtoto wako kwenye biashara ya ukahaba? Au kwa sababu nchi nyingine wanafanya hivyo kwa hiyo hiyo inamaana hata wewe ufanye? Hujui kuwa kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe? Mbona unataka kumtupa mtoto wako uliye kaa nae miezi tisa tumboni, hukumbuki ule uchungu wakati wa kujifungua? Yote hayo ulifanya bure,ili leo umuite mtoto wako Malaya,mbwa? Au unakipaji cha kutukana,kama ndio kaitukane miti basin a sio damu yako mwenyewe.
Laiti kama tungekuwa tunatembea usiku wa manane mitaani na kuona jinsi watoto wanavyopata shida kwasababu ya jamii isivyo mjali mtoto na hivyo kutompa nafasi inayostahili. Inafikia hatua hao watoto wanabatizwa majina,eti watoto wa mitaani,ni kweli ni watoto wa mitaani lakini hujui kuwa wametoka kwa baba na mama wa mitaaani pia? Unajua taabu ya kulala kwenye makorido ya nyumba za wahindi? Wewe sasa hivi unachakula na ndo maana huwezi elewa ninachokisema, nakushauri uwe makini maana haya mabo hubadilika kama upepo wa kiangazi.
Na hii eti ndo familia yake anayotakiwa kujifunza na kukua nayo, yaani kwa ujumla hi indo jamii yake ya karibu ambayo anatumia muda mwingi zaidi. Baadae wanakuja ndugu wengi na hasa kwa familia zetu za kiafrika. Udanganyifu huongezeka kadri watu wanavyozidi kuwa wengi nyumbani na hivyo ushawishi unaozidi kumfanya mtoto awe katika mazingira magumu zaidi
3. Imani na shule

Hapa mtoto huusishwa na namna fulani ya imani ya kimila au ya kisasa au dini au dhehebu fulani ili afanane na jamii hiyo. Na hapa ndio tunakutana na mambo kama ubatizo na kupewa majina yanayofanana na imani hiyo. Mtoto anapelekwa shule na mara nyingi chekechea na kuendelea. Wengine pia hupelekwa makanisani au kwenye mikusanyiko mingine ya kiimani ili kufundishwa mambo yanayouhusu imani.
Mashuleni mtoto anafundishwa elimu inayofanana na dunia hii ili aweze kuyakabili maisha na changamoto zake. Katika mambo ya imani mtoto anafundishwa mambo yasioonekana lakini ambayo ni ya msingi kuliko yanayoonekana. Anafundishwa juu ya imani ya wazazi wake hata kama inamfaa au haimfai. Utajuaje kuwa inamfaa au haimfai, wakati ambapo mtoto amekua na sasa anadhihirisha yale yote yaliondani yake na ambayo kwa hakika ndiyo aliyofundishwa. Sasa inakuwaje mzazi huyo huyo aliyemfundisha mtoto mambo hayo yote leo hii aje kusema eti watoto wa siku hizi wameharikbika kabisa?

Hapa nitaongea zaidi maana ni eneo la muhimu sana katika makuzi bora ya mtoto na ndo humjengea msingi wake wa namna atakavyokuja kuishi baadae.
4. Jamii ya ujumla

Hapa sasa ni pale mtoto anapokutana ma marafiki huko nje, anaazna kukutanana na njia mbali mbali za mawasiliano kama simu, mtandao na pia anapata taarifa nyingi zaidi. Mtoto katika jamii hii anakuwa anamaamuzi ya kuchagua vitu mbali mbali anavyovipenda, atachagua marafiki, atapata muda wa kuangali luninga katika vipindi mbalimbali vinavyoonyeshwa. Na pia anakuwa na uhuru wake wa ndani wa kufuata yale aliyoyaona na kuyasikia katika kukua kwake. Na huenda kuna mgawanyo mkubwa zaidi ya huu, huu nilioandika hapa ni mfano kwa ajili ya kuelezea kile ninachotaka kusema na ili tufike mahali tuone ni wapi panahitaji msaada ili kuhakikisha kuwa haki za mtoto zinalindwa na kutetewa.

Tuesday, September 21, 2010

Papaa On Tuesday......Unaziba Tundu La Panya Kwa Kipande Cha Mkate?

Marafiki Huru Ni,
Ni matumaini Yangu Tuko wazima kwa kudra za Bwana Wetu Yesu Kristo. Nina kila sababu ya Kumshukuru Mungu Kutupa uzima katika kipindi hiki cha Kampeni za Uchaguzi lakini Pia tukiwa tumebakiza siku 4 tuingia pale Mlimani City Kwenye “Sifa Zivume”.


Juzi na Jana kwenye account yangu Face Book alijaribu kupata mawazo kutoka kwa watu kutokana na “Case” iliyokuwa mezani kwangu tangu alhamisi Jioni. Wanawake wengi sana hawapendi kudanganywa inapofika suala la mahusiano, iwe kabla ya ndoa ama baada ya ndoa, na wakati huo huo wanaume wengi sana wanashindwa kukizingatia kile kipengele cha kiapo kinachosema “Wengine Wote Nitawaepuka na kuambatana na wewe Siku Zote” hahahaha hapo bwana, unataka kujua?fanya tathimini Wake za Watu wangapi wako active kwenye Face Book na Wanaume za Watu wangapi wako active Face book na mitandao Jamii mingine. Kituko kingine ni vile Mpendwa mmoja amemshauri mchumba wake kwa hekima ajitoe kwenye Face Book, Tagged, Hi 5 na Twitter hii yote ni Mitandao Jamii pengine atamwambia ajitoe na Marafiki Huru kwa kuwa anahisi anaweza kuibiwa na Wajanja, Mdada kwa kujali na kutunza Mahusiano akaamua kujitoa ingawa ilikuwa ina muuma lakini “Fo The Sake Of Love” akawa hapatikani huko kote. Siku Ya Alhamis sijui niseme ni Mungu ama ni Machale baada ya kutuma picha za Marafiki Huru kwenye Net na zingine kuzipost katika Face Book na kwenye Blogs akaona ni vema akaangalie hizo picha akiwa Café. Alipofika Café akashawishika kuingia Face Book, akajiweka offline ili kutunza ndoa, kuangalia kati ya watu walio online Mchumba wake yuko online, akaamua kwenda kuangalia kwenye profile and photo comments za mtu wake, mmh akakuta yule kaka yuko full huru na Wana facebook, alipojaribu kwenda kwenye accont zingine za mitandao mingine since alikuwa na password akakuta password zimebadilirishwa teh akaona kama noma na iwe noma akajiweka online akaanza kuchat na mtu wake, swali la kwanza la Jamaa, kwanini umeingia Face Book?wakarumbanaaaa. Kesi bado inaendelea kwa sasa.

Ninachotaka kusema hapa sio tu ni namna gani watu wamekuwa sio waaminifu na wala sitafuti nani ni waaaminifu kuliko wengine kwenye mahusiano. Ila ninachotaka kukisema ni namna gani kwenye maisha tunataka kufunika mambo yaonekane ndivyo kumbe sivyo na tukusahau kunasiku yatakuja kutugharimu siku yakibainika. Nitatoa mifano michache ambayo inaweza kukugharimu kama utashindwa kujiweka huru Mapema. Marafiki Huru huwa tunaambiana ukweli, pale ambapo panapaswa kusemwa. Maisha yetu ya kila siku yanawaeza yakawa ni yakulipa gharama kila iitwapo leo kwa uongo ama ukweli tuliouficha wakati Fulani tukisahau kuwa utakuja bainika, maneno yetu ya kujificha ni kama kipande cha mkate kwenye shimo la panya ambapo kuna wakati mkate utaliwa tu.

Umesikia hizi issue sijui Tumaini Sio Raia sababu ana upara, Papaa Siojui kwao ni Congo ndo maana mfupi, kuna wakati mambo yetu yatawekwa bayana. Assume wewe unafanya kazi kwa kutumia Jina sio lako ama vyeti sio vyako, na umekuwa huru sana hapo ofisini, umewahi waza siku wakasema mwenye jina kama lako ameapply kazi teh teh. Unapotumia taarifa ambazo sio sahihi katika ajira kuna saa ya kulipa taarifa hizo. Jaribu kuwaza siku rafiki huru unatolewa kwenye TV kwenye taarifa ya habari kuwa huyu Jamaa alifahamika sana kama Papaa Sebene kumbe jina lake la kweli ni Asangalwisye Kandukungonde, ukitaka kugombea ubunge watu uliosoma nao wanasema tunamjua. Unapofunika kitu leo jua kuna siku ukweli utajulikana. Kwenye CV watu mnajijazia mavitu kibao ambayo sio ya kweli ili uwashawishi Saa ipo nayo saa yaja mfuniko wako utaondolewa na utajulikana.

Aheri ya nyie ambao mmeshaoa na kuolewa hahahaha kwa sisi ambao ni Living Single changamoto bado ni nyingi na kubwa kubwa, unakuata Jambazi anajifoji anakuwa kama Sister wa kanisa Katoliki, Professional Cheater anajifoji kama Baba Mchungaji, kila mtu ajifoji huku makucha yamefunikwa. Unadhani umepata huku ndani kwa ndani mtu anajijua kabisa hili ni bomu ambalo litalipuka saa yoyote. Watu siku hizi wanapendwa kwa vitu vyao na sio kama walivyo, kuna watu wanampenda Papaa sababu ni Creative, Kuna watu wanampenda Mussa sababu anaongea Mapoint, Kuna watu wanampenda Daisy sababu she is very open, wengine wanampenda Clara kwa vile alivyo, kuna wengine wanampenda Prosper kutokana na Macho yake kila mtu anamtazamo wake katika mstakabari wa mapenzi. Unapoingia katika mahusiano ndipo unagundua hawa watu sivyo walivyo, unatumia miaka 3 kusoma mtu ambaye tabia zake ni kama maandishi ya Kiarabu ama Kichina kila unapodhani Kichina kumbe ni Kiarabu, mwisho wa siku mabomu mawili yanaamua kujilipua. Kwanini tusiwe wakweli?Biblia inasema ‘Kama Msingi Ukiharibika, Mwenye Haki atafanya Nini?tusizibe mashimo ya panya kwa vipande vya mikate. Just be open and straight kwenye kile unachokitaka na usichokitaka.
Hakuna jambo baya tena la fedheha mtu uliyekuwa unahesabika decent na una integrity yako kumbe sio ulivyo. Leo hii tukasikia Harry ile gari kumbe alimdhurumu mtu hahaha au tukasikia Addo ameshtakiwa kwa kutoa Rushwa, ama tusikie Josephine anatembea na boss wake, yaani kila ukichangia point hapa kwenye jukwaa watu watakuwa wanaongea yao moyoni. Inakuchukua dakika moja kudanganya watu zaidi ya 100 ila inakuchukua miaka kadhaa watu wale wale kukuamini tena kama walikubaini sivyo ulivyo. Ukibambwa unapoteza ujasiri, ukibambwa unahisi kila siku watu wanakuongelea wewe issue yako. Kwanini Usiwe huru?Kila unapotaka kudanganya chochote na popote just remember hiki ni kipande cha Mkate kwenye shimo la Panya. Jana nimesoma kichekesho kimoja Mchungaji alimpa rushwa Traffic, baada ya siku 2 mke wa traiffic akawa mgonjwa, mkewe akamwomba mumewe ampigie simu mchungaji wao aje amuombee, kwa kuwa baba hakuwa ameokoka alikuwa hamfahamu mchungaji wa mkewe anafananaje. Mara baadaya kuelekezana kwa simu mchungaji akawasili nyumbani kwa ile familia kufungua mlango Traffic anakutana uso kwa uso na Mchungaji, teh teh pata picha unaombaje sasa kwa mgonjwa. Hahaha inakuwa vipi changudoa uliyetembea nae jana usiku anakukuta unahubiri kanisani na mkakumbukana..hahahaha Kama wewe ni A kuwa A.

Nimalize kwa kusema kuna gharama kubwa ya kulipa kwa yale ambayo leo tunayafunika ili tuonekane ndivyo kumbe sivyo. Usifunike Kipande cha Mkate kwenye shimo la panya.


....//Papaa
http://www.samsasali.blogspot.com/

Friday, September 10, 2010

MINDSET UPGRADE:WE ARE DIVIDED NOT BY OUR DIFFERENCES

MH,Leo nawapa kutafakari only one thing:

Inaonekana kuwa sababu kubwa ya watu kutengana na kukorofisha na ni kutoelewana katika kukubaliana kwenye mambo ya msingi yanayohusu tofauti zao.Its like saying our differences should separate us just how the Britton used the divide and rule approach during colonialism. I DONT AGREE.

I AGREE THAT WE ARE NOT TO BE DIVIDED BY OUR DIFFERENCES BUT BY THE INABILITY,INCAPACITY,INCAPABILITY AND FAILURE TO RECOGNIZE,ACCEPT AND CELEBRATE AND PRAISE THE DIFFERENCES IN US NA KAMA UNABISHA ASK A MAN AND A WOMAN WHO ARE MARRIED WHAT KEEPS THEM TOGETHER GIVEN THEY HAVE EVERYTHING DIFFERENT.

JESUS UP

Tuesday, September 7, 2010

Rafiki Huru Papaa On Tuesday.....Is Not Linking But Its Links Sometimes.

Marafiki Huru natumai tuko njema tukijiandaa na Siku Ya Marafiki Huru hapo Jumamosi. Najua pressure inapanda Pressure inashuka.

Nianze kwa kusema kuna matukio mengi sana yaonayoendelea katika maisha yetu kwa kuyafanya ama kufanyishwa au kufanyisha tukudhani hayana uhusiano na sisi kwenye maisha yetu ukweli ni kwamba yanauhusiano mkubwa sana kwa jicho la karibu as if they are not linking, the fact ni kwamba yana link.

Wiki chache zilizopita tuliona Past inavyoletwa mbele ya maisha yako ya sasa na unatumia muda mwingi ku deal na past stories kuliko present na future, tazama Dr. Slaa suala la ndoa na Upadri ambavyo limeshikiwa bango he thought is not linking but its links, tangu Makamba atishiwe kusemwa hadharani kwanini alifukuzwa ualimu amekuwa na adabu amegundua kuna link na ulaji wake CCM.

Kuna mambo mengi sana tunadhani yanatokea kwenye maisha yetu by chance na tukaamua kuyapotezea lakini the fact is kuna link kubwa ya matukio ya maisha yetu ya nyuma ya sasa na wakati ujao. Wote tunatambua story ya Yusuph na ndugu zake matukio yoteeeee ukiyatazama ni kama hayana link na future yake lakini ndo scenario nzima mpaka anakuja kuwa waziri mkuu from gerezani as if is not linking but it links mtu wangu. Kaa dakika mbili think of yourself where you came from watu uliokuwa nao na kusoma nao, angalia ulikopita huwezi jua kama kuna link na future yako but I tell you there is a link.

Mimi leo nisingesoma Mzumbe ukweli idea ya Marafiki Huru isingekuwepo mpaka ikawa hivi, Kama sio Mzumbe ningemjulia wapi Protace, kama sio kuwepo Magomeni ningemjulia wapi Blandina, Kama Sio VCC ningemjulia wapi Mwombeki, Kama sio Kambi ya watoto wa Wachungaji ningemjulia Prosper Mwakitalima, Kama Sio Mgisa ningemjulia wapi Irene Lyatuu, Kama sio Rapha Kwenda anzisha fellowship angempata wapi Mkewe, kama Sio Facebook ningekutana wapi na Nietiwe, kam Sio Keziah tungempata wapi Mzee wa Uchakachuaji, Kama sio sisi wote kuwepo marafiki tungeipata wapi Marafiki Huru, Kama sio Poul Makonda ningempata wapi Edna Sichwale na Lucy Kayombo, Kama Sio Godwin Roman na Mongi ningeingiaje CU, kama sio Addo kumpisha Chen lei na kupata ajali tungepataje ushuhuda wa Addo na Mchina, these things we think they don’t link with our lives the fact is kuna li-link.

Ask yourself mara ngapi mambo mengi yanatokea kwako ndo unakuja realize kuna connection, huwezi Jua Mungu anataka Marafiki Huru Ifike wapi but there must be a link and connection with our future. Waza mwenyewe namna ulivyojiunga na kanisa ulilosali, waza namna ulivyopata kazi, waza namna ulivyompata mume au mkeo, waza namna ulivyopata nyumba unayokaa, kuna link kubwa sana, ninachotaka kukuthibitishia it doesn’t matter what are you passing though, the best is yet to come, ukitazama ulivyo sasa na ulikotoka as if there is no link but ipo, maisha ni ups and down getting and loosing, our future is already designed. Kuna watu wanakuja kwenye maisha yetu wanatuuuuuuuumizaaaaaaaaaaaaa, but good enough they are just part of our future. Usitazame kidole kinachoonesha mwezi utazame mwezi wenyewe.

Nimejifunza kujisikia vibaya pia ni sehemu ya maisha, usijisikie vibaya kujisikia vibaya, there other times I feel lonely and alone, lakini kuna neno huwa nalitumiaga na Protace tangu tukiwa mwaka wa kwanza chuoni, Hili nalo Litapita, nakumbuka kulikuwa na hard times kwenye maisha yetu ya chuo, tulikuwa mpaka kuna majira ya kukusanya na kupotezea, nakumbuka Protace alilazwaaaa hahahah Jamani Mapenzi balaaaaa yaani unapenda mpaka unalazwa dhuuu, na tulipobaki wawili tu tukiwa tunaongea tunakuliza kwanini hili limetokea, then tukasema “Hili Nalo Litapita”. Some other times Mungu anawaondoa people we loved them very much yaani kama nilivyompendaga naniiiiiii, lakini we see kama ulimwengu wote umekwisha, unawazaaaaaaa hupati majibu, ukweli ni kwamba its just a Season, huwezi kupotezea siku zote, there is a time you will get what you want. Hahahahah we better loose Helen and Getting Anna, kama sio Mate wa Irene Lyatuu Kumwaga Naniii, Glory angepatikana wapi?
Nimalize kwa kusema historia inaweza kuandikwa kwa dakika moja na isifutike milele na unaweza dhani is not linking but it links someday somewhere. Huwezi kuwa na hali zote siku zote, huwezi kuwa na furaha siku zote, usijisikie vibaya kujisikia vibaya, kupata na kukosa vyote kwenye maisha vipo, huwezi kupata milele kuna siku utapoteza, huwezi kuwa nafuraha kuna siku watu watakuboa, huwezi kufurahishwa na MH siku zote, lakini hakuna anayeweza kudumu kwenye hali moja siku zote, kila linalotokea katika maisha “Jua Nalo Litapita”

If two people always agree on everything, then one of those people is probably not needed…..Is not linking But It Links.
…//Papaa

Monday, September 6, 2010

WANAFUNZI WANYIMWA UHURU WA KUABUDU



msikiti wa alzahra ndani ya chuo kikuu zanzibar
 Chuo kikuu cha Zanzuibar(Zanzibar University) chavyunja katiba ya zanzibar kwa kuwanjima uhuru wa kuabudu wafunzi wa kikirsto wa  chuo kikuu cha Zanzibar…katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kipengele cha 19(1) na 20(1) ….na kile cha katiba ya Tanzania 1977 kipengele cha  19(1) na 20 (1)…
Mwaka jana  28 december  makamu wa rais wa chuo cha zanzibar alipiga  maarufu mkusanyiko wowote wa kikirsto ndani ya maeneo ya chuo…wakati huohuo kukiwa na misikiti miwili hapo chuoni
Hili limepelekea kukamatwa kwa muunjilisti Peter Masanja mwezi iliyopita mwaka huu…masanja ambaye alipotea ghafla..iligundulika amekamatwa baada ya mkewe kumtafuta kwa siku kadhaa..masanja ambaye ni mkazi paje wa Zanzibar alikamatwa  kwa kosa la kufundisha mwafunzi wa kikirsto chuoni wapo
Wanafunzi wa kikirsto wana mpango wa kwenda mahakamani kupinga kunyimwa uhuru wa kuabudu..Chuo hicho kimewatishia kuwafukuza wasichana wa kikirsto kama hawatavaa hijabu


Sunday, September 5, 2010

NDOA YA UPENDO NKONE MWEZI 10

Muimbaji wa Injili Upendo Nkone atategemea Kufunga ndoa tarehe 17 October 2010 na Mchungaji John Mbeyela ambaye pia ni mjane mwenye watoto watatu, ndoa hiyo itafungwa katika kanisa la Naioth kwa Mchungaji Mwasota.
Akiongea na Strictly Gospel Upendo Anasema “Ninafurahi sana na ninaomba Mungu akamfute machozi kila mjane, haijalishi umekaa miaka mingapi. Mungu yupo atakukumbuka”
Bi. Nkone ambaye ameishi maisha ya ujane kwa miaka 9, ana jumla ya album tatu ambazo ni Mungu Baba, Hapa Nilipo na Zipo faida.
Tunamtakia kila la heri katika maandalizi yote mpaka arusi!

Friday, September 3, 2010

JUANITA KUTOA ALBUM YA MAISHA YAKE

Yule mwinjilisti maarufu na muumbaji   Rev. Juanita Bynum is not finished sharing her story and hopes to inspire others.
Bynum, who lives in metro Atlanta, recently signed with the Houston-based World Music Entertainment empire, headed by Mathew Knowles.
Her new album, “The Diary of Juanita Bynum” is scheduled for release in 2011. She said the trilogy project is not going to be just “another CD, but it’s going to be a message and the story of my heart and my diary.”
Hii album  itakuwa inaelezea maisha yake…magumu aliyopitia baada ya kuachwa BAADA ya  kupigwa mbele za watu na mume wake BISHOP THOMAS W. WEEKS III mwaka 2007
 

Thursday, September 2, 2010

MINDSET UPGRADE:THE DIFFERENCE WE SHARE WHEN WE THINK DIFFERENTLY

Dear MH,

There is a difference that we share when we think differently.Yes.You cant think differently and remain the very same person with old fashioned thinking and lifestyle.You cant think differently and live uninformed life,remember any decision based on little information will be a shameful experience to you.What am I saying today? I say,WE ARE DIFFERENT,we think differently,talk differently, different lifestyle, different preferences,different systems of beliefs,different tastes of things,you see eveything is different.

So our difference doesnt mean our separation.Namaanisha kuwa utofauti wetu haimaanishi tutengane bali tuungane kwa ukaribu zaidi.Practically,this is different also.Watu wakitofautiana kitu wanatengana,hiyo iko kila eneo kuanzia kanisani, mtaani,mpaka ikulu.WHY,because of kitu kinaitwa SELFISH ATTITUDE.Ulishawahi kujiuliza kwanini watu wanataka kuoa huku wote wawili wanatofautiana kila kitu?But it seems that its their difference that makes them come together and not separate.

This means,when we share the difference we have,there is a way we are going to think very different and as such our mindset will be impacted to reveal the positivity which is positive for ourselves and the nation.

YOU CANT THINK DIFFERENT AND REMAIN THE VERY SAME PERSON.

10 Points and commandments in Human Relationship that can help you think differently,share your difference and make a great deal of differences in life.

1. Speak to People
There is nothing like a cheerful word of greeting. To really connect, look them in the eye as you speak.

2. Smile at People
It takes 72 muscles to frown, only 14 to smile. They can hear the difference in your voice - even over the phone.

3. Call People by Name
The sweetest music to anyone's ear is the sound of his/her own name. Be sure you say it correctly. Say it often.

4. Be Friendly and Helpful
To have friends and build relationships, be a friend first.

5. Be Cordial
Sincerely speak and act as if everything you do is a genuine pleasure.

6. Be Genuinely Interested In People
You can like almost everybody if you try. They don't care how much you know until they know how much you care. Be sure they know how much you care.

7. Be Generous With Praise
Praise publicly, correct privately. Everyone wins this way.

8. Be Considerate of the feelings of others. There are usually three sides to a controversy: yours, the other person's, and the right side. Keep ego and emotions in check.

9. Be Alert
To give excellent service. What counts most is what we do for others not ourselves.

10. Have a Good Sense of Humor
Don't take yourself too seriously. When you add lots of patience, and humility, you will have a recipe for enduring success.

JESU UP

MAREKANI INAVYOBADILIKANA NA KUWA NCHI YA KIISLAM


In
1952
President  Truman

Established  one  day  a  year  as  a

"
The National Day of Prayer.

------------------------------------------
 
In
1988
President Reagan
Designated the
First Thursday in May of each year as

The National
Day of Prayer

 

In June

2007
(then)

Presidential
Candidate Barack Obama

Declared that the USA

"Was no longer  a
Christian nation." 

------------------------------------------------------

 This year
President Obama

Canceled the
21st annual National Day

Of Prayer ceremony

At the White
House under the ruse
Of "not wanting to offend anyone"

-------------------------------------------------------

BUT... On September 25, 2009
From 4 AM until 7 PM,
A National Day of Prayer
FOR THE MUSLIM RELIGION
Was Held on Capitol Hill,
Beside the White House.
There were over 50,000 Muslims
In  D.C. That da
OBAMA AKIINGIA KUSWALI
 y
.  


Wewe ni Bwana - Enid Moraa

Wednesday, September 1, 2010

REBEKA KUZINDUA ALBUM JUMAPLI

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka kwaya ya Kindondoni Revival anajulikana sasa kwa jina la Rebecca Lukule Nzelwa sasa anakuja na album yake binafsi mbali na kundi la kwaya anayoimba.

Album ni ya kumrudishia Mungu sifa na shukrani, inaitwa MUNGU NAKUSHUKURU WEWE NI MTETEZI WANGU ina jumla ya nyimbo 8, na itawekwa Wakfu Siku Ya tarehe 5 September 2010, Kanisani kwao Kinondoni Revival Church.

MH LWENDO NA MSEGU NDANI CASUAL WEAR SUNDAY

Msegu akiimba kwa hisia
 Katika kuumalizia mwezi wa kusifu na kuabudu mwaka huu, Calvary temple   ya Arusah jumapili iliyopita kulikuwa na  na ibada ya kusifu na kuabudu na  mavazi yalikuwa  casual wear  ili kuwakaribisha wale ambao wangetamani kuja kanisani lakini wanafikiri kanisani ni sehemu ya mavazi maalum!!rafiki huru Msegu alikuwepo kwenye safu ya kuongoza nyimbo na Godlove Lwendo alikuwa kwenye Gitaa
Msegu ya pili kulia

Tuesday, August 31, 2010

Papaa On Tuesday Kama Haipo Haipo Tu!Ila Sio Rahisi Kuipotezea


Marafiki Huru hope tuko pouwa, Mara nyingi tumezoea ule msemo wa “Kama Ipo Ipo Tu” yaani kwa maana ya kwamba kama kitu ni cha kwako ni cha kwako hata ikiwaje, lakini tumesahau kabisa kuwa kuna wakati mwingine haipo na haipo kweli lakini tunahitaji hicho kitu ama mtu kwenye maisha yetu ya kila siku. Ukweli unabaki kuwa ipo lakini hatuwezi kuipata na tunahitaji iwe yetu huwezi ipotezea wakati mwingine tunajifarii kama ipo ipo lakini ukweli hiyo tunayoikosa inatuuma na sio rahisi kuipotezea kana kwamba ulikuwa huitaki.

Kuna watu tumetamani sana wawe wenzi wetu kwenye maisha na wengine walifanyika marafiki wazuri sana lakini ghafla mambo yakageuka yakawa ndivyo sivyo je unapotezea?kwa kusema kama ipo ipo?kuna wakati haipo na tunaihitaji kwa wakati huo. Tukiwa chuo nilimpendaga sana yule dada aliyekuwa nyuma mwaka mmoja, Protace aliyekuwa rafiki yangu anakumbuka sana mahusiano yangu na yule dada, wazee wa fellowship akina Rapha, Tangi J, david, Msegu, Mbarikiwa na Sebene group lote walikuwa wameanza mchukulia mama mtumishi, hahahaha Addo pamoja na Tumaini ndo waliokuja kuniambia Papaa umeingia ndiko siko kwa issue moja mbili tatu, baada ya ufuatiliaji wa issue moja mbili tatu nikabaini nimeingia choo cha kike ukweli unaachilia huku bado unahitaji unapetezea wakati bado inakuuma? Then unajifariji kama ipo ipo tu lakini kuna wakati haipo na tunaihitaji kwenye maisha. Ukikaa mbele za watu kana kwamba umeachia na unapotezea ukikaa mwenyewe just alone unagundua kama haipo kweli haipo lakini kupotezea sio rahisi.

Kuna wakati tunatamani tuhame katika ofisi tunazofanyia kazi kutokana na manyanyaso mbali mbali mengine toka kwa waajiri wetu na wengine wafanyakazi wenzetu, umewahi takwa na bosi wako??kama hujawahi usiombe zahama hiyo ikukute, kuna wakati unaumiaaaaaa, kuna wakati unaliaaaaaaa, lakini huwezi ondoka ukasema kama ipo ipo tu why?unajua kamabisa ikiwa haipo huwezi ipotezea bwana pamoja na shida lakini ndo ndo ndo si chururu. Kuna wakati tunatamani wengine kutoka kwenye relationship tulizoingia lakini kweli utoke kwa jeuri ya Kama ipo ipo?thubutuuuuuu, ikiwa haipo huwezi potezeakuwa sawa na ikiwepo. Inawezekana haijawahi kukuta tatizo kubwa kwenye maisha yako ndo maana unaongea kama utakavyo, umewahi waza siku unapofanyia kazi ukiambiwa kuwa kuanzia leo hauna kazi tena utaondoka na kuwaambia watu kama ipo ipo?lakini ukikaa mwenyewe chumbani huwezi ipotezea kuwa eti ipo unagundua kuwa ikiwa haipo huwezi jifanya ipo bado unaihitajikwa kiasi kikubwa tu kwenye maisha. Umewahi waza mchumba wako ama mpenzio siku akifa ama amkiachana kwa namna yoyote ile utajipa moyo kuwa kama ipo ipo?unaweza ukawa unajipa moyo kwenye macho ya watu but still huwezi kuvumilia moyo unaumaaaaaaaaa, kwa sisi tulio wahi experience kukataliwa katika ku-approach tunafahamu namna ambavyo sio rahisi kupotezea moyoni kuna mchakato mahususi “to let it go”. Sio rahisi kupokea taarifa ya mkeo ana ujauzito wa rafiki yako, rafiki yako unayefanya nae biashara amekula capital ya biashara baada ya kumwamini na kumpa then ukasema kama ipo ipo ...kuna wakati tunaikosa wakati tunaihitaji iwepo.
Jiulize mambo mangapi mpaka sasa yamekuwa yakikutesa wewe mwenyewe kwa kujifanya unapotezea eti kama ipo ipo lakini ukikaa mwenyewe na ukikumbuka kichwa kinazunguka na kukuuma mpaka unatamani kulia ama wengine hata kufa, ukikumbuka fedha ulizopoteza, ukikumbuka muda uliopoteza, ukikumbuka ulivyojiotolea kwa kiasi kikubwa...watu wakikuona unasema kama ipo ipo tu...but kumbuka umeshindwa ipotezea kwa sababu ukweli wa moyo kama haipo huwezi ipotezea kimya tu.

Kama ipo Ipo tu! Lakini kama Haipo Sio Rahisi Kuipotezea.

Think Differently and Make a Difference.


…//Papaa